Friday 22 February 2013

VIDEO YA TRACK MPYA YA OFFSIDE TRICK NA BABY J-USINIPE


COUNTY COMMISSIONER GARISSA:SERIKALI IPO IMARA KATIKA SWALA LA USALAMA WA GARISSA

County commissioner wa Garissa Bw Mohamed maalim amesema kuwa serikali ipo imara katika maswala ya usalama katika kaunti ya Garissa.Maalim amesema kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa usalama wa wakaazi wa Garissa umeimarishwa vilivyo huku akiwaomba wakazi wa Garissa kutoa habari zozote kwa maafisa wa usalama, na pia wakome kuwaficha wahalifu.Aidha maalim alisema kuwa kulingana na upelelezi ni kwamba zipo hospitali za kibinafsi zinazotoa huduma kwa wahalifu kwa kuwapatia matibabu wanapopata majeraha katika shughuli zao za uhalifu.Maalim amesema hospitali zitakazopatikana na makosa ya kuwatibu wahalifu zitafungwa mara moja.Pia amewahimiza wanainchi wa Garissa kuhakikisha kuwa wanadumisha amani haswa wakati huu tunapoelekea kwa uchaguzi huku akionya kuwa watakaozua vurugu watakiona cha mtema kuni kwani mkono wa sheria utakabiliana nao vilivyo.

ONYO KWA WAKAAZI WA GARISSA KUTOKA KWA MZALENDO KIBUNJA

Mwenyekiti wa tume ya uwiano na maridhiano NCIC Bw. Mzalendo kibunjia amewaonya wakaazi wa Garissa dhidi ya Ubaguzi wa kikabila,akizungumza katika mkutano  na wakaazi wa kaunti ya Garissa hapo jana.Mzalendo kibunjia alisisitiza kwamba ubaguzi wa wakenya haswa wale ambao si wa asili ya kisomali ni jambo ambalo halifai na linafaa kukemewa kabisa.Katika hotuba yake kibunjia aliwaomba wanainchi wa Garissa kupuuza matamshi ya baadhi ya watu na viongozi yanayosambaratisha uhusiano mzuri uliopo kati ya wakenya walio na asili ya kisomali na wale wasiokuwa wasomali huku akisema kuwa wakenya wanafaa kuwa mstari wa mbele kuheshimu na haki na maslahi ya kila mtu.