Thursday 30 October 2014

MAANDAMANO BURKINAFASO



Rais wa taifa la Burkina faso Blaise Compaore ametangaza hali ya dharura na kuvunjilia mbali serikali ya taifa hilo baada ya maelfu ya wanainchi kuandamana na kuchoma majengo ya bunge.Maandamano hayo yaliyotokea alhamisi ya tarehe 30 Novemba yamesababishwa na  mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa ili kumruhusu rais wa taifa hilo  kubakia mamlakani kwa muhula mwingine.waandamanaji hao walivamia kituo cha televisheni cha taifa pamoja na majengo mengine ya serikali.Ni maandamano yaliyosababisha takriban watu wawili kupoteza maisha huku rais akitangaza hali ya dharura na  kuitisha mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kutafuta suluhisho ya hali ilivyo.Kufikia sasa hali ya taharuki inazidi kushuhudiwa katika taifa hilo.

UTAYARISHAJI WA VIDEO MPYA NA KWANZA YA KIGOTO MMBONDE



Utayarishaji wa video inayosubiriwa na wengi ya wimbo wa msanii kigoto mmbonde tayari ushaanza. Mashabiki wa msanii huyo wanafaa kutazamia makubwa kutoka kwa msanii huyo ikizingatiwa kuwa hii ndio video ya kwanza kabisa kutoka kwa msanii huyo.Kigoto ni msanii ambae kufikia sasa ametatiza saana na vibao kama vile vumilia,kichapo cha mapenzi,ridhika na aire.Kulingana na meneja wa kigoto ambae pia ni msanii Susumila ni kuwa baada ya utayarishaji wa video ya aire kukamilika,kigoto atakua anaachia wimbo wake mpya.Video ya Aire inatayarishwa na kampuni ya CMG FILMS kampuni ambayo ilitayarisha video ya Susumila-hidaya.