Tuesday 8 December 2015

JE MSANII KIGOTO YUKO WAPI?..JE KUNA UGOMVI WOWOTE KATI YAKE NA TK2 MSIKILIZE HAPA AKITIRIRIKA

Ni mmoja kati ya wasanii wenye vipaji vya hali ya juu na amewahi kuvuma kwa vibao kama vile kichapo cha mapenzi,ridhika vumilia,Napenda vizuri miongoni mwa ngoma nyingi kali zenye ubora wa hali ya juu saana katika upande wa utunzi,ushairi na sauti ya kipekee ambayo imemuwezesha kujizolea mashabiki wengi kwa kipindi cha mda mfupi.Kwa kipindi cha mda sasa Kigoto amekua kimya kiasi tangu aachilie kibao chake cha napenda vizuri na mashabiki wengi wamekua wakijiuliza yuko wapi?Je kuna ugomvi kati yake na producer TK2? Je ni lini anaachilia kibao kipya?Sababu ya kukaa kimya ni ipi?...Huyu hapa kigoto msikilize akizungumzia mipango yake ikiwemo projects alizoziandaa,Management yake mpya pamoja na kuweka wazi uhusiano wake na producer wake Hit maker TK2.
 http://www.audiomack.com/song/mtubei-media/kigoto-azungumzia-mipango-yake-pamoja-na-uhusiano-wake-na-tk2
BONYEZA HAPA KUMSIKILIZA KIGOTO

Wednesday 26 August 2015

MZIKI WA SIKU HIZI HAUNA CHA UNDERGROUND WALA MKONGWE,WOTE SAWA




Muziki wa siku hizi hauna cha mkongwe wala underground kama huamini uliza wakongwe flani ambao kwa sasa wanatapa kufa maji.ukijiita underground ni kujidharau mwenyewe.Kinachotofautisha wasanii siku hizi ni bidii na kipaji na sio ukongwe na umaarufu.Kama wasemavyo wahenga kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake,naona pia mtaji wa msanii yoyote ni kipaji na bidii yake.

Zamani kidogo miaka flani ya nyuma kupenya na kuitawala sanaa ilikua rahisi saana kwa sababu ya ufinyu wa ushindani uliokuwepo.Miaka hiyo ambapo sanaa ndio ilikua inajitengenezea jiwe la msingi,msanii alikua anaweza kuimba kitu chochote na watu wakamkubali.Miaka hiyo pia ni wakati ambapo msanii alikua anaweza kutawala chats na wimbo mmoja kwa takriban miaka mitatu akipiga shows na kubaki gumzo kwa midomo ya wengi kwa kipindi kirefu.Hukuhitajika kama msanii kuwekeza pesa nyingi kwa video za ubora kama ilivyo sasa ili ufanye vizuri.Wakati huo pia katika vipindi vingi vya redio hakukua na ushindani mkubwa vile kwa hivyo ilikua ni rahisi wimbo wako Kukubalika kupenya na kutawala vipindi.Mambo yoote haya yaliruhusu dhana flani itawale katika fikra za wengi,dhana hii ikiwa ni kuamini kuwa kizuri chatoka tu kwa wale wasanii ambao washatengeneza jina tayari.Dhana hii ilipelekea wasanii wengi wachanga kukanyagiwa na nafasi nyingi kupewa wasanii ambao wamejipatia umaarufu tayari.Hapo ndio nahisi kuwa jina la underground lilipotokea.

Kizazi kilichofuata kikawa kizazi cha kuhonga ili kuwezesha mziki wako kuchezwa redioni.Kwa sababu kwa kipindi hicho mziki ulikua bado mchache sokoni,sanaa ilinajisiwa kwa kiwango flani kwani wadau wengi walilazimisha mziki flani sokoni kisa hongo.Wasanii wengi waliweka imani kuwa ili kufanikiwa katika sanaa lazima uhonge Dj au presenter ili waweke kazi zao hewani.Kipindi hiki cha mda kilishuhudia kushuka kwa viwango vya mziki kwani mziki m’bovu ulitawala saana na kulazimishiwa mashabiki huku mziki mzuri ukikanyagiwa.Kwa kiwango flani ,wengi wa washikadau ilikua kuuweka mziki wako hewani ilikua ni lazima utoe hela au kama wewe ni msanii wa kike ilikua ni lazma ugawe utam ili mziki wako uwekwe hewani.

Tunafaa kushkuru kwa sasa maana kizazi tulicho nacho sasa mambo yameanza kubadilika.Ushindani uliopo kwa sasa umesaidia saana katika kuhakikisha kuwa shabiki anatambua sifa za mziki mzuri.Mifumo mingi iko ambayo imempa shabiki nguvu ya kujua kubainisha kizuri na kibovu.Katika kizazi cha sanaa tulicho nacho kwa sasa,kama ulikua umezoea kuhonga kama msanii basi utahonga saana maana hali imebadilika.Tofauti na zamani siku hizi presenters na ma DJ ni wengi kiasi kwamba presenter flani akibania msanii kwingine msanii huyo huyo anapewa shavu la kiuhakika na kama mziki wake mzuri,utajitangaza wenyewe.Katika kizazi hiki pia, platforms  za kujitangaza ni nyingi saana ikiwemo mitandao ya kijamii ambapo msanii anaweza kusambaza na kutangaza kazi zake na aka hit bila msaada wa Dj wala PRESENTER.Mimi binafsi msanii shembwana masauti nilimjua mtandaoni na nikatafuta kazi zake zote baada ya kuskia wimbo wake mmoja nilioupenda na hadi sasa bado namfuatilia .Siku hizi mtu wa kuhongwa sio presenter na Dj tena bali ni shabiki,hivyo basi kila msanii anaumiza kichwa amhonge shabiki na sio kwa pesa bali ni kwa kupitia mziki mzuri.Katika kizazi hiki ukiwa na kipaji ukijiita underground ni kujidharau maana kila siku wasanii wachanga wenye vipaji wanachipuka na kupitia kazi zao nzuri,mashabiki wanawakubali na kupelekea kuwapa wakongwe ushindani sokoni.Inapendeza kuona kwamba siku hizi wasanii waliochipukia juzi tu wanatumbuiza jukwaa moja na wasanii wakongwe, sio kama curtain raisers bali kama wasanii waliojizolea umaarufu kupitia talanta,ubunifu na bidii.

Pongezi ziende kwa wasanii wakongwe kama vile,Nyota ndogo,ali b,amour baby,susumila miongoni mwa wengine kwa kuhimili ushindani uliopo kwa sasa maana wako wengi ambao wamepotezwa kwenye game kisa ushindani balaa uliopo.Kwa mara ya mwisho,mziki wa siku hizi hauna underground.Talanta,bidii na mpangilio ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya msanii.

Sunday 19 July 2015

NEW VIDEO:NUMBER ONE ACADEMIA-NIKO NAWE


SARATANI INAYOUA MZIKI WA PWANI

Ni kwa siku nyingi saana mziki wa pwani umekua kaburini na unazidi kutapatapa kujitoa uonekane katika hatua za juu.Wengi wamejiuliza ni kipi kinachosababisha hali hii huku kukiwa na hali ya kurushiana lawama ila kulingana na upeo wangu mdogo wa mziki nilionao nahisi kwamba kila mshikadau kuanzia producer,watangazaji na ma DJ,wasanii wenyewe hadi mashabiki wote wamechangia katika hali hii.
MASHABIKI.
Labda nianze na shabiki,Ni kwa mda mrefu saana sasa msanii wa nyumbani amelalamika saana kwamba wewe shabiki unamnyima nafasi kwenye skio lako na kwamba nafasi hiyo umewapa wasanii wa magharibi mwa africa pamoja na marekani.Hii ni hali ambayo msanii wa pwani imezidi kumkatisha tama sana.Kufikia kiwango cha msanii Kaa La Moto kutunga wimbo uliokemea hali hii na kumhimiza kila mkenya kiujumla kuukumbatia na kuukubali mziki wa nyumbani kwanza kabla kuupa nafasi mziki wa mataifa mengine.Kwanza pongezi kwa msanii KAA LA MOTO kwa wimbo KLM IS DEAD,pili kwa tatizo hili lawama itaanguka popote pale iwe kwashabiki,presenters,DJS,Maproducer miongoni mwa washikadau wote katika sanaa. Anayebisha kuwa pwani hakuna vipaji ni muongo au kiufupi tuseme tu ana laana maana kwa upeo wangu mdogo wa muziki nilionao naweza kusimama mbele ya watu na kujivunia vipaji vya wasanii kama Ally BJohnny Skani,Dazlah Kiduche,Majid,Susumila,Amoury beyby,Dogo Richie,Kaa la Moto,Nyota Ndogo,Lovemums, Jovial,Kigoto Mmbonde,Alkenia Love,Shaah Biggy,Chikuzee,Shembwana Masauti,Fisherman,Canibal,Sharama,Mchafuzy, Sudi Boy, Lai miongoni mwa wasanii kibao tu ambao kila siku wanakesha wakijaribu kila wanaloliweza kutupatia kazi nzuri na kuuweka mziki wa pwani katika ramani ya kitaifa na kimataifa kiujumla.
Ninachoamini ni kuwa wasanii wetu japo sio wote bali wengi wao wana nia hivyo basi sisi kama mashabiki.Tukiwapa sapoti ni dhahiri kuwa itawapa moyo wa kufanya bidii kuimarisha sanaa hii na kufikia viwango vya kupendeza kila skio.Sijasema kuwa ususie kazi nzuri za wanamziki wa inje ya pwani,  hapana....ninachomaanisha ni kuwa tusiwe watumwa wa kiakili kupenda zaidi vya wenzetu kufikia kiwango cha kudharau kazi nzuri za wasanii wa hapa kwetu.
Nafasi iko kubwa ya kuimarisha uchumi wa sanaa yetu ya nyumbani na kabla nizungumzie fursa hizo kwanza kila shabiki anafaa kutambua kuwa sanaa ya kila msanii iko kwa mikono ya yeye shabiki,hivyo ina maana kubwa kuwa msanii hata awe na bidii kiasi gani bila shabiki ni dhahiri atafeli tu,maana katika kila kazi anayotoa msanii,ni lazima shabiki apate kuiskia,aipende na aipitishe moyoni mwake.Pia tunafaa kuelewa kuwa kumkubali na kumsifia msanii pekee hakutamuekea chakula mezani wala kumuimarisha kisanaa,shabiki anachofaa kutambua ni kwamba sanaa ni kazi wala sio ngazi ya kutengeneza maskini wenye umaarufu.Hivyo basi ni utovu mkubwa wa shukrani,unafik na kukosa uzalendo kama shabiki hatampa sapoti msanii wa nyumbani na kuhamisha sapoti hiyo kwa wasanii wa kigeni.Hapo ndio tunarudi tena katika zile fursa za kuukuza uchumi wa soko letu la mziki ambazo nimekudokezea hapo awali.
Naam,shabiki unafaa kutambua kuwa kwa kununua kazi za msanii,iwe ni kwa mfumo wa ulbum au mifumo ya kidijitali kama vilemkito,mdundo, miito ya simu pamoja na mifumo yote ya mitandao kunampa mapato makubwa saana msanii.Pia wewe kama shabiki ukijitahidi kuhudhuria matamasha ya wasanii wa nyumbani ni kitu kinachompa nguvu sana msanii na kumtengenezea maslahi yanayomuongezea mbolea katika safari yake ya mziki maana ni kupitia mapato haya ndio watajibidisha hata kujitangaza nnje ya pwani kupitia bidii ya kutoa mziki mzuri na video zilizo na ubora wa kimataifa.

MAPRESENTER NA MA DJ 
Hawa ni washikadau wawili ambao ni nguzo kubwa saana katika mziki maana ndio wanaotegemewa na msanii kufikisha kazi kwa mashabiki na pia vilevile shabiki amewekeza uaminifu wake kwa wawili hawa kujua kwamba akihitaji mziki mzuri atakua anaupata kila siku kupitia kwao.Sanaa ikidondondokea pua lawama kubwa itawaendea wawili hawa,endapo sanaa itaimarika basi ni wazi kuwa asilimia kubwa ya sifa itawarudia wawili hawa.Naheshimu saana juhudi za DJs na PRESENTERS ila ujumbe unaofaa kuwaendea ni kwamba mziki m'bovu ni m'bovu tu hata uchezwe mara milioni kwa siku.Hakuna kitu kibaya kama kuona mziki unadidimia kila siku wakati mziki mzuri unanyimwa nafasi hewani huku mziki m'bovu ukipewa nafasi kisa upendeleo au mtu hongo.Ni picha ya kusikitisha kuona chat za top ten zikitawaliwa na nyimbo mbovu ambazo hata mtoto mdogo zitampatia uvivu wa kuzisikiliza kwa ubovu wake kisa mtu kahonga au pengine anapewa teke la "ushkaji".Hii ni hali inayouregesha mziki nyuma kwani ni utahira wa hali ya juu kuleta mazao yaliyooza sokoni tukiacha bidhaa nzuri zikiozea shambani.Ile siku DJ na PRESENTERwataweka tamaa kando na kuanzisha harakati za kuupa nafasi mziki mzuri na vipaji halisi hewani,hapo tutakua tumepiga hatua kubwa saana katika safari ya kuufikisha mziki wetu mbali.Kwa mtazamo wangu,upendeleo,ushabiki na "ushkaji" ni saratani kali saana inayoua mziki kwa kasi kubwa na wanaofaa kutibu saratani hii ni ma DJ pamoja na ma PRESENTER.Kivipi? kwanza kabisa kazi mbovu ni mbovu tu iwe imetoka kwa msanii mkubwa au mdogo,kama mtu amechemsha,amechemsha tu na anafaa kurekebishwa tuweke ushabiki kando,pili kuna watu wanaimba tu kisa mjombake au ndugu yake ni DJ au Presenter wa radio flani akijua wazi kwamba atapata shavu la kutoka kimabavu hata kama kipaji sufuri. 
Upendeleo kama huu ukiuweka pembeni itakua tumepiga hatua nyingine kubwa katika safari yetu ya mafanikio.Kwa mara nyingine nasisitiza kuwa pwani hakuna uhaba wa mziki mzuri, hivyo basi hakuna sababu inayopelekea mziki m'bovu kulazimishiwa maskio ya shabiki wakati kuna kazi nyingi nzuri zinazohitaji nafasi katika soko letu la burudani. Tatu,Sioni sababu presenter kuupa asilimia kubwa mziki wa mataifa ya magharibi katika kipindi chake na kuitupa jalalani CD ya msanii wa nyumbani mwenye kipaji ambacho hakitaburudisha tu mashabiki wa nyumbani bali pia kitapandisha uchumi wa sanaa yetu kwa kiwango kikubwa.Ni kwa mara nyingi saana ma presenter mbalimbali wamejitokeza na kukiri kuwa wanalazimika kuucheza mziki wa mataifa ya nnje kwa kisingizio kuwa mashabiki huupendelea saana mziki huo zaidi ya ule wa nyumbani.Huu naweza kusema kuwa ni uongo wa hali ya juu kwani shabiki kwa mara nyingi huzibwa macho na hao ma presenter na kuaminishwa kwa nguvu kuwa wasanii wa nyumbani ni "kanjanja".
Hali hii hupelekea mashabiki kulazimishwa kuamini kuwa kizuri pekee ni kile kigeni.Tunafaa kuelewa kwamba hao wasanii wageni ambao tumewahusudu saana walipewa sapoti na kukubalika kwao kwanza kabla waote mbawa za kuja kuusambaza mziki wao huku kwetu. Hivyo basi tunafaa pia sisi tuondoe nidhamu ya uoga,tujiamini na kile tufanyacho,tujitahidi kwa pamoja ili wasanii hao wageni wakija kwetu kujinadi pia sisi tuwe na vigezo vya kwenda kujinadi huko kwao kwa kuuza kile kizuri tulichonacho.Hii yote italetwa na juhudi za DJ na PRESENTER kuwapa sapoti wasanii bora na sio bora wasanii.Mwiba wa mwisho ni huu hapa.Mtangazaji hafai kujivika maringo mbele ya msanii,anachofaa kutambua ni kuwa sanaa imemsaidia saana katika kazi yake.Utagundua kwamba mziki ni muhimu kwako wewe mtangazaji endapo utavuta taswira ya kipindi cha top ten bila muziki.hivyo basi mtangazaji elewa kuwa asilimia flani ya pato lako liko mikononi mwa msanii.  

MSANII
Sasa hapa ndio shina kuu la sababu ya makala haya lilipo.Kabla tuendelee namnukuu prof jay kwenye wimbo wa mtazamo akisema"sioni sababu za msingi kuomba kwenye mitaa,kama una kipaji iweje ufe na njaa?" ila katika wimbo huo huo pia namnukuu afande selle akisema "hivi ni lazima sote tuwe wasanii,mimi nadhani imetosha wengine tuwe mashabiki".Hii inaonesha wazi kwamba kila mmoja ana haki ya kuwa msanii kwani mziki hauna mwenyewe,ila wasanii ni wengi ila wachache saana ndio wenye vipaji.Talanta ni kitu cha msingi saana ambacho mtu anafaa kukitambua mapema saana katika safari ya maisha yake.Inasikitisha kuona wasanii wengi wenye tungo dhaifu wanalazimisha kitu ambacho ni dhahiri kuwa hawajahesabiwa na mungu kisa ubishoo.Msanii yoyote ambaye yuko kwenye mziki kutafta umaaarufu anafaa kujua kuwa anaishi katika upande usiofaa wa historia.Tunafaa kuelewa kuwa hata uwe na nia kiasi gani kama talanta huna ya kuimba rudi nyumbani ukajifikirie tena ni talanta gani ambayo mwenyezi mungu alikupa,kwani umaarufu ambao unautafuta kwenye mziki unapatikana katika talanta zingine kwani kuna watu dunia hii wamejenga jina na kuishi maisha mazuri kupitia uchoraji na hata kupiga marimba. mwaka juzi kuna msanii kutoka kundi la MAKEKE FAMILY kwa jina RUDIWUU alitoa dis track ambayo ilielekezwa kwa ma presenter inayoitwa HAKI NA USAWA na kuiweka you tube.Kwenye ngoma ile RUDIWUU aliwatusi ma presenter wengi mashuhuri matusi ya nguoni kwa kuwataja majina mmoja baada ya mwingine akidai kuwa wanawanyanyasa wasanii wa nyumbani kwa kutowapa airplay.Kwa mtazamo wangu wimbo ule kama ulikua unawakilisha kilio cha wasanii wa pwani basi ni aibu kubwa saana kwa sanaa ya pwani kuwa na mabalozi kama wale.Kwanza kabisa wimbo ulikua unaitwa "HAKI NA USAWA". Ni haki gani hiyo anayoizungumzia?

 Tunafaa kujua kuwa sio haki ya msanii kuchezwa kwa radio station,ingekua ni haki basi kesi zingekua zimejaa kortini au barabara zingekua haziishi maandamano.Sote tunafaa kuelewa kuwa katika hii safari Producer,msanii,presenter,DJ na shabikitunategemeana.Tunafaa kuelewa kuwa stesheni za runinga na redio vipo kibiashara,kujuza na kuelimisha huku fungu la msanii la kuburudisha likija mwisho kabisa.Mziki na burudani vinatumika tu kama kivutio kwa wasikilizaji.Hii inaonyesha wazi kuwa mmiliki atachagua kinachovutia kwa wasikilizaji wake ili kukidhi mahitaji ya ushindani mkubwa uliopo sasa katika sekta ya burudani na uanahabari.Jukumu lote hili la kuchagua kilicho bora kwa skio la msikilizaji linaanguka kwa mikono ya presenter.

Hivyo basi wewe kama msanii unafaa kuwajibika pia katika harakati zako za kutoa mziki mzuri ambao utakua unamsaidia yule mtangazaji pamoja na DJ kujenga jina kwa yule shabiki wanayemlenga.Kuna msemo unao sema asiyefanya kazi naasile,vilevile msanii ambaye hatajitahidi katika ubunifu hafai kuwa na nafasi katika skio la shabiki.

MSIKILIZE DAZLAH AKIZUNGUMZIA MZIKI WAKE PAMOJA NA COLLABO YAKE NA MSANII MKUBWA WA NAIROBI

Msanii kutoka studio ya TEE HITS kwa jina la DAZLAH KIDUCHE huenda ikawa sio kichwa kigeni katika skio lako kama wewe ni mfuatiliaji makini wa mziki wa pwani.Msanii huyu mwenye umri mdogo saana amechipuka na kukua kwa kasi ya juu saana katika tasnia ya mziki wa pwani na kufikia sasa, licha ya kuwa ni msanii aliyeanza mziki miaka ya juzijuzi,kwa wakati huu amewapiku baadhi ya magwiji na kuandikisha jina lake katika orodha ya wasanii wachache wanaowakilisha mziki wa pwani kitaifa na kufikia sasa tunaweza kusema kimataifa
Katika siku za hivi majuzi msanii Dazlah ameonekana kuwa mmoja ya wale wasanii wanaojituma saana na kuwekeza kwenye mziki kuanzia upande wa studio,mauzo pamoja na kazi zenye akili ili kukidhi mahitaji ya soko gumu la muziki.

Huyu apa dazlah msikilize akizungumzia mengi kuhusu mziki wake, siri ya mafanikio yake pamoja na collabo yake na msanii mmoja maarufu wa Nairobi.
 bonyeza hapa kumskiliza LISTEN

SABABU ZA ELIANO MTALIANO KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA

Ukiwa ni mwaka wa uchaguzi Tanzania,kumetokea wasanii wengi wa mziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji kujitokeza na kutumia umaarufu walionao  kugombea nyadhifa mbali mbali za kisiasa inchini Tanzania.Wasanii hawa ni kama vile a Prof Jay,Keisha pamoja na waigizaji steve nyerere na wema sepetu.
Inaonekana hali kama hii huenda ikadhihirika wazi hapa pwani kwani ikiwa ni mapema saana msanii wa injili kutoka hapa pwani anayekwenda kwa jina mtaliano eliano amejitokeza na kuweka wazi azma yake ya kuingia kwenye siasa mwaka wa 2017....huyu hapa msikilize akizungumzia ngazi ya kiti atakachogombea,eneo analopania kusimamia pamoja na sababu zake za kujitosa kwenye siasa.