Muziki wa
siku hizi hauna cha mkongwe wala underground kama huamini uliza wakongwe flani
ambao kwa sasa wanatapa kufa maji.ukijiita underground ni kujidharau
mwenyewe.Kinachotofautisha wasanii siku hizi ni bidii na kipaji na sio ukongwe
na umaarufu.Kama wasemavyo wahenga kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake,naona
pia mtaji wa msanii yoyote ni kipaji na bidii yake.
Zamani
kidogo miaka flani ya nyuma kupenya na kuitawala sanaa ilikua rahisi saana kwa
sababu ya ufinyu wa ushindani uliokuwepo.Miaka hiyo ambapo sanaa ndio ilikua
inajitengenezea jiwe la msingi,msanii alikua anaweza kuimba kitu chochote na
watu wakamkubali.Miaka hiyo pia ni wakati ambapo msanii alikua anaweza kutawala
chats na wimbo mmoja kwa takriban miaka mitatu akipiga shows na kubaki gumzo
kwa midomo ya wengi kwa kipindi kirefu.Hukuhitajika kama msanii kuwekeza pesa
nyingi kwa video za ubora kama ilivyo sasa ili ufanye vizuri.Wakati huo pia
katika vipindi vingi vya redio hakukua na ushindani mkubwa vile kwa hivyo
ilikua ni rahisi wimbo wako Kukubalika kupenya na kutawala vipindi.Mambo
yoote haya yaliruhusu dhana flani itawale katika fikra za wengi,dhana hii ikiwa
ni kuamini kuwa kizuri chatoka tu kwa wale wasanii ambao washatengeneza jina
tayari.Dhana hii ilipelekea wasanii wengi wachanga kukanyagiwa na nafasi nyingi
kupewa wasanii ambao wamejipatia umaarufu tayari.Hapo ndio nahisi kuwa jina la
underground lilipotokea.
Kizazi kilichofuata
kikawa kizazi cha kuhonga ili kuwezesha mziki wako kuchezwa redioni.Kwa sababu
kwa kipindi hicho mziki ulikua bado mchache sokoni,sanaa ilinajisiwa kwa
kiwango flani kwani wadau wengi walilazimisha mziki flani sokoni kisa
hongo.Wasanii wengi waliweka imani kuwa ili kufanikiwa katika sanaa lazima
uhonge Dj au presenter ili waweke kazi zao hewani.Kipindi hiki cha mda
kilishuhudia kushuka kwa viwango vya mziki kwani mziki m’bovu ulitawala saana
na kulazimishiwa mashabiki huku mziki mzuri ukikanyagiwa.Kwa kiwango flani ,wengi wa washikadau ilikua kuuweka mziki wako
hewani ilikua ni lazima utoe hela au kama wewe ni msanii wa kike ilikua ni
lazma ugawe utam ili mziki wako uwekwe hewani.
Tunafaa
kushkuru kwa sasa maana kizazi tulicho nacho sasa mambo yameanza
kubadilika.Ushindani uliopo kwa sasa umesaidia saana katika kuhakikisha kuwa
shabiki anatambua sifa za mziki mzuri.Mifumo mingi iko ambayo imempa shabiki
nguvu ya kujua kubainisha kizuri na kibovu.Katika kizazi cha sanaa tulicho
nacho kwa sasa,kama ulikua umezoea kuhonga kama msanii basi utahonga saana
maana hali imebadilika.Tofauti na zamani siku hizi presenters na ma DJ ni wengi
kiasi kwamba presenter flani akibania msanii kwingine msanii huyo huyo anapewa
shavu la kiuhakika na kama mziki wake mzuri,utajitangaza wenyewe.Katika kizazi
hiki pia, platforms za kujitangaza ni
nyingi saana ikiwemo mitandao ya kijamii ambapo msanii anaweza kusambaza na
kutangaza kazi zake na aka hit bila msaada wa Dj wala PRESENTER.Mimi binafsi
msanii shembwana masauti nilimjua mtandaoni na nikatafuta kazi zake zote baada
ya kuskia wimbo wake mmoja nilioupenda na hadi sasa bado namfuatilia .Siku hizi
mtu wa kuhongwa sio presenter na Dj tena bali ni shabiki,hivyo basi kila msanii
anaumiza kichwa amhonge shabiki na sio kwa pesa bali ni kwa kupitia mziki
mzuri.Katika kizazi hiki ukiwa na kipaji ukijiita underground ni kujidharau
maana kila siku wasanii wachanga wenye vipaji wanachipuka na kupitia kazi zao
nzuri,mashabiki wanawakubali na kupelekea kuwapa wakongwe ushindani sokoni.Inapendeza
kuona kwamba siku hizi wasanii waliochipukia juzi tu wanatumbuiza jukwaa moja
na wasanii wakongwe, sio kama curtain raisers bali kama wasanii waliojizolea
umaarufu kupitia talanta,ubunifu na bidii.
Pongezi ziende
kwa wasanii wakongwe kama vile,Nyota ndogo,ali b,amour baby,susumila miongoni
mwa wengine kwa kuhimili ushindani uliopo kwa sasa maana wako wengi ambao wamepotezwa
kwenye game kisa ushindani balaa uliopo.Kwa mara ya mwisho,mziki wa siku hizi
hauna underground.Talanta,bidii na mpangilio ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya
msanii.