Wednesday, 26 September 2012
MTOTO MCHANGA WA UMRI WA TAKRIBAN MWEZI NA NUSU APATIKANA AMETUPWA CHOONI HUKO NEP TECHNICAL GARISSA
Wanafunzi wa NEP TECHNICAL GARISSA wamepigwa na mshangao asubuhi ya leo baada ya kupata mtoto wa kike mchanga wa takriban mwezi na nusu ametupwa chooni kwenye shule hiyo.inadaiwa kuwa mwanafunzi mmoja alikuwa ameenda haja kujisaidia aliposkia sauti ya mtoto mchanga analia ndani ya shimo la choo hicho.Hapo ndipo mwanafunzi huyo aliomba msaada kwa wenzake ambapo walisaidiana kuvunja choo na kumuokoa mtoto huyo.Kufikia sasa haijabainika kama ni mtu wa nje alitekeleza kitendo hicho au ni mwanafunzi,hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo wametaja kuwa hawajashuhudia mwanafunzi yoyote akiwa na uja uzito aliyejifungua na kuishi na mtoto kwenye shule hiyo.mtoto huyo sasa amechukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya mkoa ya Garissa.Kisa hiki kinajiri takriban mwaka mmoja baada ya kijusi kupatikana kimetupwa jalalani katika mtaa wa bula kartasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment