Wednesday, 26 September 2012

MWANAUME MMOJA AHUKUMIWA KIFO KATIKA MAHAKAMA YA GARISSA

Mwanaume mmoja kwa jina ISMAEL MARATA amehukumiwa kifo na mahakama ya Garissa kwa kupatikana na hatia ya  kosa la wizi wa mabavu.
ISMAEL MARATA anadaiwa kutekeleza wizi huo katika tarafa ya MADOGO, kaunti ya TANA
RIVER. akitoa hukumu yake,Hakimu wa mahakama hiyoBI, NDUNG'U alisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa dhidi ya mshtakiwa, na pia kujitetea kwa mshitakiwa, ilibainika wazi kwamba ISMAEL MARATA alitekeleza kitendo hicho cha uhalifu.
Katika mahakama hio hio mwanaume mmoja kwa jina DEMELESH AMBAW KEBEDE raia wa ethiopia amepatikana na hatia ya kuwa Kenya bila kibali.amepigwa faini ya shilling 80,000 ama atumikie kifungo cha miezi nane gerezani. DEMELESH ambaye alikubali makosa yake, alikamatwa tarehe 25 mwezi SEPT  katika kizuizi cha BANGALE.Vile vile katika mahakama hiyo-hiyo mwanaume kwa jina la ABDULLAHI ABDI alikabiliwa na mashtaka ya mauaji katika tarafa ya Madogo, kaunti ya TANA RIVER. hakimu BI, NDUNG'U ameagiza mshitakiwa azuiliwe korokoroni kwa siku saba hadi polisi watakapo kamilisha uchunguzi.ABDULLAHI ABDI anakumbwa na tuhuma za kumuua shemeji yake.

No comments:

Post a Comment