Friday, 28 September 2012

GARISSA LET US TOGETHER MAKE OUR TOWN CLEAN



                                          TUSITUPE TAKATAKA OVYO,UCHAFU HULETA
                                           MAGONJWA
                                    



                                          USAFI WA JIJI UNAANZA NA MIMI NA WEWE

JINSI MAMBO YALIVYOKUA KATIKA MKUTANO WA WASANII MTAANI MJINI GARISSA

                                               JUSTICE THE BOSS AKILISHA NENO KWA 
                                               WASANII
                                             G KREW,G CLAN,VIP,JUSTICE,DJ SAFO WA
                                             CLUB MOMBASA  RAHA WALIKUEPO
                                                        SAFARI MUSEMBI WA WARSAN
                                                              F.M PIA ALIKUWEPO


                                            TUKAPATA FREESTYLE KUTOKA KWA JUSTICE




Mkutano wenyewe ulienda poa na lengo la mkutano huo ilikua ni kufufua Entertainment industry ya Garissa na Tana river ili kuhakikisha kuwa wasanii wa kimuziki,spoken word,drama,dancers na vijana wengi walio na vipaji mbalimbali waweze kujipatia kitu kutokana na vipaji vyao

TUKAKUTANA NA WANAFUNZI WA GARISSA ACADEMY

                                          POZ  LA KWANZA
                                          POZ LA PILI

Wednesday, 26 September 2012

MTOTO MCHANGA WA UMRI WA TAKRIBAN MWEZI NA NUSU APATIKANA AMETUPWA CHOONI HUKO NEP TECHNICAL GARISSA

Wanafunzi wa NEP TECHNICAL GARISSA wamepigwa na mshangao asubuhi ya leo baada ya kupata mtoto wa kike mchanga wa takriban mwezi na nusu ametupwa chooni kwenye shule hiyo.inadaiwa kuwa mwanafunzi mmoja alikuwa ameenda haja kujisaidia aliposkia sauti ya mtoto mchanga analia ndani ya shimo la choo hicho.Hapo ndipo mwanafunzi huyo aliomba msaada kwa wenzake ambapo walisaidiana kuvunja choo na kumuokoa mtoto huyo.Kufikia sasa haijabainika kama ni mtu wa nje alitekeleza kitendo hicho au ni mwanafunzi,hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo wametaja kuwa hawajashuhudia mwanafunzi yoyote akiwa na uja uzito aliyejifungua na kuishi na mtoto kwenye shule hiyo.mtoto huyo sasa amechukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya mkoa ya Garissa.Kisa hiki kinajiri takriban mwaka mmoja baada ya kijusi kupatikana kimetupwa jalalani katika mtaa wa bula kartasi.

Manchester United 2-1 Newcastle

Mabao mawili kutoka kwa anderson na cleverly yawezesha Manchester united kuidondosha newcstle chini huku Papiss Cisseakiifungia Newcastle bao la pekee

ARSENAL 6-1 COVENTRY

Oliver Giroud aifungia arsenal bao lake la kwanza katika ushindi mkubwa wa mabao 6-1 arsenal ilijipatia dhidi ya Coventry. Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Andrey Arshavin, Theo Walcott na Ignasi Miquel huku bao la kufutia machozi la coventry likifungwa na Callum Bell.

MWANAUME MMOJA AHUKUMIWA KIFO KATIKA MAHAKAMA YA GARISSA

Mwanaume mmoja kwa jina ISMAEL MARATA amehukumiwa kifo na mahakama ya Garissa kwa kupatikana na hatia ya  kosa la wizi wa mabavu.
ISMAEL MARATA anadaiwa kutekeleza wizi huo katika tarafa ya MADOGO, kaunti ya TANA
RIVER. akitoa hukumu yake,Hakimu wa mahakama hiyoBI, NDUNG'U alisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa dhidi ya mshtakiwa, na pia kujitetea kwa mshitakiwa, ilibainika wazi kwamba ISMAEL MARATA alitekeleza kitendo hicho cha uhalifu.
Katika mahakama hio hio mwanaume mmoja kwa jina DEMELESH AMBAW KEBEDE raia wa ethiopia amepatikana na hatia ya kuwa Kenya bila kibali.amepigwa faini ya shilling 80,000 ama atumikie kifungo cha miezi nane gerezani. DEMELESH ambaye alikubali makosa yake, alikamatwa tarehe 25 mwezi SEPT  katika kizuizi cha BANGALE.Vile vile katika mahakama hiyo-hiyo mwanaume kwa jina la ABDULLAHI ABDI alikabiliwa na mashtaka ya mauaji katika tarafa ya Madogo, kaunti ya TANA RIVER. hakimu BI, NDUNG'U ameagiza mshitakiwa azuiliwe korokoroni kwa siku saba hadi polisi watakapo kamilisha uchunguzi.ABDULLAHI ABDI anakumbwa na tuhuma za kumuua shemeji yake.

Tuesday, 25 September 2012

PINI KALI KUTOKA KWA SAMIR FT DULLY SYKES-SINA RAHA


HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA MH WILLIAM RUTO KWA PAGE YAKE YA FACEBOOK

Kumbuka kuna tetesi zilikuepo kuwa mheshimiwa william ruto alikuwa amelazwa akiugua ugonjwa usiojulikana lakini huyu hapa mwenyewe namnukuu kupitia page ya ke ya facebook amesema "I was scheduled to leave the country Sunday for business after a successful function in Kajiado . That evening I had a routine appointment with my dentist Proff Guthua which ordinarily would last 20min . My plans however changed when the Dentist decided to carry out a minor surgery which was quick and successful. Now am recovering and will be up n running in 2-3 days. Thank you for ur moral support n prayers and sorry for the conflicting information."

VICTOR WANYAMA"NAFURAHI SAANA KUICHEZEA CELTIC"

Baada ya vilabu kadhaa kutoka uingereza kummezea mate,kiungo wa kati wa klabu ya celtic victor wanyama kwa sasa ametoa kauli yake na kusema kuwa kwa sasa anazingatia kwa saana mkataba alionao kwa sasa na klabu hiyo.kulingana na kauli ya yake namnukuu“I leave things like a contract to the club and my agent but I am really happy here and looking forward to staying for many years,” says Wanyama

COLLABO YA CAMP MULLA NA WIZKID YATOKA

Track kali iliyosubiriwa na wadau wengi wa mziki africa mashariki kutoka kwa wakali wa style ya 254 CAMP MULLA wakimshirikisha msanii kutoka nigeria WIZKID kwa sasa ishatoka.Katika track hiyo msanii wizkid amechukua verce ya kwanza na ameweka mbali uwezo wake wa kuchana na akaamua kuweka ladha ya uimbaji kidogo.Track hiyo imejumuishwa katika ulbum ya CAMPMULLA iliyotoka juzi inayokwenda kwa jina la FUNKYTOWN.Katika ulbum yao hiyo,CAMPMULLA pia wamewashirikisha wasanii kadhaa kama vile bamboo,collo,J-Smilez,na Just A Band ..usichelewe kujipatia copy yako kwani mzigo uko madukani tayari

Monday, 24 September 2012

AVRIL ASHINDWA KUFANYA COLLABO NA A.T

huyu binti kwa jina la AVRIL kashindwa kufanya kolabo na AT msanii kutoka zanziba kisa ameshindwa kuimba style ya mduara ambayo kwa saana AT anaitumia.....duuuh ikabidi safari ya AT kutoka tanzania kuingia kenya kwa lengo la kufanya collabo na avril ikaingia doa na ikambidi AT kumtafuta mtu mwingine kufanya naye kolabo hiyo