Friday, 22 February 2013

COUNTY COMMISSIONER GARISSA:SERIKALI IPO IMARA KATIKA SWALA LA USALAMA WA GARISSA

County commissioner wa Garissa Bw Mohamed maalim amesema kuwa serikali ipo imara katika maswala ya usalama katika kaunti ya Garissa.Maalim amesema kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa usalama wa wakaazi wa Garissa umeimarishwa vilivyo huku akiwaomba wakazi wa Garissa kutoa habari zozote kwa maafisa wa usalama, na pia wakome kuwaficha wahalifu.Aidha maalim alisema kuwa kulingana na upelelezi ni kwamba zipo hospitali za kibinafsi zinazotoa huduma kwa wahalifu kwa kuwapatia matibabu wanapopata majeraha katika shughuli zao za uhalifu.Maalim amesema hospitali zitakazopatikana na makosa ya kuwatibu wahalifu zitafungwa mara moja.Pia amewahimiza wanainchi wa Garissa kuhakikisha kuwa wanadumisha amani haswa wakati huu tunapoelekea kwa uchaguzi huku akionya kuwa watakaozua vurugu watakiona cha mtema kuni kwani mkono wa sheria utakabiliana nao vilivyo.

No comments:

Post a Comment