Rais wa taifa la Burkina faso Blaise Compaore ametangaza hali ya dharura na
kuvunjilia mbali serikali ya taifa hilo baada ya maelfu ya wanainchi kuandamana
na kuchoma majengo ya bunge.Maandamano hayo yaliyotokea alhamisi ya tarehe 30 Novemba
yamesababishwa na mabadiliko ya katiba
yaliyopendekezwa ili kumruhusu rais wa taifa hilo kubakia
mamlakani kwa muhula mwingine.waandamanaji hao walivamia kituo cha televisheni
cha taifa pamoja na majengo mengine ya serikali.Ni maandamano yaliyosababisha
takriban watu wawili kupoteza maisha huku rais akitangaza hali ya dharura na kuitisha mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kutafuta suluhisho ya hali ilivyo.Kufikia
sasa hali ya taharuki inazidi kushuhudiwa katika taifa hilo.
Thursday, 30 October 2014
UTAYARISHAJI WA VIDEO MPYA NA KWANZA YA KIGOTO MMBONDE
Utayarishaji wa video inayosubiriwa na wengi ya wimbo wa msanii kigoto mmbonde tayari ushaanza. Mashabiki wa msanii huyo wanafaa kutazamia makubwa kutoka kwa msanii huyo ikizingatiwa kuwa hii ndio video ya kwanza kabisa kutoka kwa msanii huyo.Kigoto ni msanii ambae kufikia sasa ametatiza saana na vibao kama vile vumilia,kichapo cha mapenzi,ridhika na aire.Kulingana na meneja wa kigoto ambae pia ni msanii Susumila ni kuwa baada ya utayarishaji wa video ya aire kukamilika,kigoto atakua anaachia wimbo wake mpya.Video ya Aire inatayarishwa na kampuni ya CMG FILMS kampuni ambayo ilitayarisha video ya Susumila-hidaya.
Subscribe to:
Posts (Atom)