Rais wa taifa la Burkina faso Blaise Compaore ametangaza hali ya dharura na
kuvunjilia mbali serikali ya taifa hilo baada ya maelfu ya wanainchi kuandamana
na kuchoma majengo ya bunge.Maandamano hayo yaliyotokea alhamisi ya tarehe 30 Novemba
yamesababishwa na mabadiliko ya katiba
yaliyopendekezwa ili kumruhusu rais wa taifa hilo kubakia
mamlakani kwa muhula mwingine.waandamanaji hao walivamia kituo cha televisheni
cha taifa pamoja na majengo mengine ya serikali.Ni maandamano yaliyosababisha
takriban watu wawili kupoteza maisha huku rais akitangaza hali ya dharura na kuitisha mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kutafuta suluhisho ya hali ilivyo.Kufikia
sasa hali ya taharuki inazidi kushuhudiwa katika taifa hilo.
No comments:
Post a Comment