Wednesday, 19 June 2013
GAWASCO YATAFUTA SULUHISHO LA SHIDA YA MAJI MADOGO
Kampuni ya kusambaza maji mjini Garissa, GAWASCO, iliandaa mkutano na wakazi wa Madogo hapo jana. Ni Mkutano ulio-andaliwa katika hoteli moja eneo la Madogo, uliokuwa wa kutafuta suluhisho mwafaka kwa tatizo la maji, ambalo limekuwa likisumbua wakazi wa Madogo kwa mda mrefu.
Kati ya maswala yalioibuka ni swala tata la kulipa maji, yaani, BILLING, huku wakazi wakiomba mbinu mpya ibuniwe ya kulipisha maji. Kuhusu malipo ya maji ya jumla, yaani FLAT RATE, meneja wa biashara wa GAWASCO, bwana Abdirahim Sheikh Hassan alisema kwamba wateja ambao hawajapata maji, elhali malipo yao ni FLAT RATE, hawatalipia billi ya maji kwa wakati ambao hawajapata maji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment