Moto uliyo teketeza sehemu ya soko Mugdi mjini Garissa huenda ukawa ulisababishwa na makaa ya moto ambayo hayakuwa yamezimwa.
Hii ni kwa mujibu wa wafanyi biashara wa soko hilo tulio zungumza nao. Mkasa huo wa moto uliotokea siku ya jumatatu usiku, uliteketeza mali ya thamani kubwa. …
Hata ingawa haijabainika haswa chanzo cha moto huo, baadhi ya wafanyi biashara walioadhirika na moto huo, walisema kuwa mfanyi biashara mmoja ambaye hupika na kuuza chakula cha Githeri hakuzima gunia la makaa aliyoyanunua, kwani hakufahamu kuwa makaa hayo, yalikuwa bado yanawaka moto.
Hii ni mara ya pili sehemu ya soko mugdi kuchomeka kwani mwaka uliopita soko hilo lilichomwa katika rabsha na mshike-mshike ya ukosefu wa usalama. Hii ilikuwa baada ya wanajeshi wawili kuwawa karibu na maeneo ya hospitali kuu ya Garissa.
No comments:
Post a Comment