Monday 22 October 2012

KARIBU TENA TANA GARDEN HOTEL GARISSA























HALI ILIVYO KATIKA MTAA WA WINDSOR MJINI GARISSA




                                                HII NI BARABARA YA WINDSOR
                                                    HII NI COMPOUND YA MTU

                               HAPO SASA IKIFIKA HAJA KITAMBO UFIKE MSALANI NI BAALAA
Ni kwa mda sasa wakaazi wa mtaa wa windsor mjini Garissa wamelalamikia kuvuja kwa kwa mabomba ya maji taka(sewerage)kufikia sasa hali imekua mbaya saana kama unavyoona kwenye picha hapo juu ambapo sewerage hiyo imefikia kiwango cha kufurika hadi kuingia majumbani mwa watu haswa baada ya mvua kubwa iliyonyesha juzi.Kulingana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao nilipata fursa ya kuongea nao ni kwamba sewerage hiyo imekuwa shida kubwa saana kwa eneo hilo kwa mda sasa na inatoka katika louge moja iliyoko katika eneo hilo.Wakaazi hao wamesema wamewasilisha malalamishi kwa wamiliki wa nyumba ili ujumbe ufike katika afisi za town council ya Garissa ili swala hilo lishughulikiwe ila juhudi zao hazijafua dafu,Baadhi ya wakaazi wanasema kuwa mwenye louge hiyo ni mtu ambaye anajulikana na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa saana mjini Garissa.

Kufikia weekend iliyopita sewerage hii ilikua imefunga kabisa barabara na imetapakaa katika ploti kadhaa za makaazi.Uvundo unaotoka katika eneo hilo umezidi huku wenyeji wakihofia kuchipuka kwa magonjwa mbali mbali yanayotokana na maji machafu.Kwa sasa wakaazi wa eneo hilo wanaomba msaada kwa washikadau wa idara husika haswa town council na Gawasco  kuingilia swala hilo ili hali ya usafi irejeshwe katika mtaa huu kwani hofu kubwa ni pale mvua kubwa itakaponyesha huenda sewerage ikaingia mpaka majikoni.

Thursday 18 October 2012

SWALA LA VITAMBULISHO GARISSA NA MADOGO LACHUKUA MKONDO MPYA

Hili swala la vitambulisho sasa naona limeanza kuchukua mwelekeo mpya.Katika maeneo mengi Garissa,Mororo,madogo,tana river county na Garissa county kiujumla,kumekua na lalama kila uchao kuwa kupata kitambulisho ni balaa.Swala hili limekua likisumbua watu wengi saana haswa wakati huu  usalama umezorota ambapo wewe kama mkenya maisha ya Garissa bila kitambulisho ni balaa.Tukiweka hayo ya usalama kapuni jambo lingine la msingi ni kuwa uchaguzi mkuu unakaribia na endapo mkenya huna kitambulisho basi inamaanisha wazi kuwa hutaweza kupiga kura.

Wiki hii kumekua na pilka nyingi saana haswa sehemu za madogo na mororo kuhusu swala hili la vitambulisho baada ya jamaa mmoja kupiga simu siku ya jumanne katika kipindi cha BURUDANI KIKWETU Katika stesheni ya SIFA F.M na kutaja majina ya watu kadhaa kwamba walimlazimisha kulipa shilingi mia mbili ndio apewe kitambulisho.Swala hili limezua mjadala mkali na ilibidi tuweze kupata kauli ya D.O kuhusu jambo hilo ambapo alitaja kuwa huduma za kupata kitambulisho ni bure na hana habari yoyote kuhusu ada ya mia mbili inayotajwa kutozwa kwa wanaotafuta kitambulisho.

Siku ya alhamisi wazee kadhaa wanaohusika na maswala ya vitambulisho walifika katika afisi za Sifa f.m ili kuweka mambo wazi kuhusu swala hili la vitambulisho ambapo walisema kuwa wanajua wazi kwamba kupewa kitambulisho ni bure ila hao kama wazee walikaa na wakaunda kamati itakayoshughulikia swala hilo la vitambulisho,hivyo basi mtu yoyote anayetaka kitambulisho itambidi alipe shilingi mia mbili kama malipo kwa ile kamati,nanukuu mmoja akisema"HIYO PESA NI KAMA MAKARIBISHO TU YA ILE KAMATI,YAAANI TUSEME NI KAMA CHAI TU AU LUNCH"mwisho wa nukuu.Walipoulizwa huwa wanamsaidia vipi mtu anayetaka kufanya vetting na hana pesa,wazee hao walisema kuwa mtu ambaye hana mia mbili na anataka kuingia vetting huwa wanamsaidia mwisho anapata kitambulisho kwani kutoa hizo mia mbili sio lazima ni hiari ya mtu.

Baada ya wazee hao kutoka,kama sadfa kukaja kijana  katika Afisi za sifa f.m aliyesema namnukuu akisema"PESA TULITOA KUANZIA MWANZO NI MIA TATU MWANZO TULITOA MIA MOJA TUKAPEWA FORM TENA KWA VETTING TUKATOA MIA MBILI KWA JUMLA HIYO NI MIA TATU,NA HIZO PESA TULILAZIMISHWA KUTOA KWA SABABU WENGINE ILIBIDI WAACHE KITU KAMA SIMU HIVI NDIO WAWEZE KUHUDUMIWA HAPO KWA VETTING WAKIMALIZA WALETE PESA NDIO WACHUKUE SIMU ZAO"mwisho wa nukuu......
 Je mkweli ni nani katika sakata hii?
 hivyo ndio hali ilivyo kuhusu maswala ya vitambulisho kwa mengi zaidi ungana na Enos Changulo ndani ya changamka Sifa f.m 101.1 upate mengi kuhusu swala hili

UKULIMA KATIKA KINGO ZA MTO TANA

Leo tukajipata MCHELELO FARM moja ya mashamba yaliyoko kando ya mto tana.Tumetambua huko maskani maswala na ukulima yamepewa kipau mbele saana.Washkaji kibao wanautumia vizuri mto tana ndio maana licha ya jua kali linalowaka tana river na Garissa kiujumla bado kuna uwezekano wa kupata mimea mingi saana ikifanya vizuri katika maeneo haya yaliyo kando na mto na hata yale yaliyombali iwapo tutakumbatia ukulima wa unyunyiziaji maji kutoka mto huo.Kulingana na hali ilivyo katika kingo za mto tana ni kwamba vipo vipande vingi saana vya ardhi ambavyo endapo vitatumiwa vizuri basi tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo ya Tana river na Garissa litapungua kwa kiwango kikubwa saana.Ndani ya mchelelo farm kuna mimea mingi saana kama vile sukuma,mchicha,mabiringanya,mabamia/mabenda,Tomato,mahindi,ndizi,vitunguu,miwa na mimea mingi saana ikiwa ni dhihirisho kubwa kuwa ardhi hii iko na rutuba ya kutosha kuweza kuhimili ukuaji wa mimea mingi tofauti.Hata hivyo kila kizuri huwa hakikosi changamoto kwani mbali na kuwepo kwa unawiri mzuri wa mimea tatizo ni kwamba zao lao mara nyingi huharibika shambani kwa sababu wa uosefu wa wanunuaji kwani eneo hilo ni mbali saana na sokoni hivyo basi zao linapokua tayari mara nyingi huozea shambani kwani kulifikisha sokoni huwa ni ngumu saana...HIZI HAPA BAADHI YA PICHA ZA ENEO HILO

TANA RIVER


                                                                NDIZI
                                                                          MIWA
                                                                PUMPKINS
                                                                      VITUNGUU
                                                              MAHINDI
                                                     MABIRINGANYA
                                                       TOMATO
                                                                  SUKUMA
                               NIKAAMUA PIA KUPOZ NA WAKULIMA WENYE 
                                               KUSABABISHA  USTAWISHAJI HUU

Sunday 14 October 2012

TANA GARDENS HOTEL GARISSA WELCOME ALL

Nyote mnakaribishwa Tana Gardens Hotel Garissa.Kama wewe ni mkazi wa Garissa hoteli hi inapatikana katikati ya kituo cha mafuta cha heller na na kituo cha mabasi cha muhsin.Kwa wale hamjawahi kufika Garissa basi hoteli hii iko mahali peupe kabisa ambapo ni rahisi kabisa kupaona au unapofika katika kituo cha heller basi utaelekezwa.Katika hoteli hii  utapata vyakula vingi na vizuri haswa vile vya kienyeji kutoka katika kila pembe ya Taifa letu ambavyo vimetayarishwa na wapishi stadi kutoka kila pembe ya Kenya.Huduma katika hoteli hii ni za hali ya juu saana.Pia kuna sehemu za makongamano na mikutano iwapo pengine una mkutano wako.Maandhari ya hoteli hii ni mazuri,tulivu na ya kuvutia saana.Karibu Tana Gardens hotel uje ufurahie huduma bora na vyakula vitamu kwa bei nafuu

Friday 12 October 2012

KISIMA AWARDS NOMINEES 2012

Artiste / Group of the Year:
Octopizzo
Daddy Owen
Nameless
Camp Mulla
Nonini
Video of the Year Category:
Nonini – Colour Kwa Face
Nameless – Coming Home
Daddy Owen – Mbona
Juliani – Exponential Potential
Rabbit – Swahili Shakespeare
Collaboration of the Year:
Alicio / Juliana
P-Unit / Sauti Sol
Daddy Owen / Denno
Longombas / Mr. Vegas
Keko / Madtraxx
Boomba Artiste Category:
Avril
Amileena
DNA
GrandPa Family
Habida
Prince Davis
Q Tasi
Mejja
Size 8
Hip Hop Category:
Nonini
Juliani
Octopizzo
Gospel Artiste of the Year:
Daddy Owen
Eko Dydda
Eunice Njeri
Mastar Piece
Emmy Kosgei
Willy Paul
Ragga/Reggae Category:
Longombas
Fireson
Kevo Yout
Wyre da Lovechild
Daddy Owen
Urban Artiste / Group Category:
Just a Band / Nonini
Camp Mulla
Boneless
Muthoni the Drummer Queen
Yvonne Darko
Nariki
Fusion Artistes Category:
Wahu
Anto Neosoul
Dan ‘Chizi’ Aceda
Sanaipei
Juliet
Judith Bwire
Benga Artiste of the Year:
Judith Bwire
Kamande wa Kioi
Wa Kahalf
Otieno Aloka
Wa Othaya
Vincent Ongidi
Upcoming Artiste of the Year:
Anto Neosoul
Camp Mulla
Nariki
Xtatic
Yvonne Darko
Alicio
East African Recognition:
Jackie Chandiru
TMK
Chameleone
Diamond
Lady Jay Dee / Mr. Blue
Professor Jay
Dynamiq

MZIGO WENYEWE SI KITAMBO UTAKUA TAYARI JO

                              MHUSIKA NA DESIGNER WA MZIGO WENYEWE ZABU ZABLON



   MJUKUU WA AKIDAH AKA MP,AKA NDEGE KASORO MABAWA AKA KELVIN AKA    MAJINA MENGI

WATOTO WAWILI WAZAMA KATIKA MTO TANA KARIBU NA MORORO

Shughuli za uokoaji bado zinaendelea katika mto tana karibu na mororo baada ya watoto wawili kuzama walipokuwa wakiogelea hapo jana mwendo wa saa kumi.Aidha kwa sasa mwili wa mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa takriban miaka tisa umepatikana hii leo majira ya asubuhi.Kulingana na taarifa,watoto hao wawili walizama katika mto huo walipokua wakiogelea.Hata hivyo shughuli za kumtafuta mtoto mwingine ambaye bado hajapatikana bado zinaendelea

Thursday 11 October 2012

HOFU YA MACHIFU GARISSA KUHUSU MFUMO WA KAUNTI

Machifu wa kaunti ya Garissa leo walikongamana katika afisi za wilaya ya Garissa kulalamikia hatima yao wakati serikali za kaunti zitakapoanza kufanya kazi.Aidha machifu hao walielezea hofu yao ya kuwa serikali huenda ikatupilia mbali kazi zao punde tu serikali za kaunti zitakapoanza kazi.Hata hivyo machifu hao wanataka wadhifa wao ubainishwe wazi kikatiba kama vile wadhifa wa kamishna wa kaunti unavyotambuliwa na wanainchi kote inchini

Wednesday 10 October 2012

K LYN AJIFUNGUA MAPACHA WA KIUME

Mrembo aliyewahi kuwa miss Tanzania Jackline ntuyabaliwe maarufu kama K lyn ambaye pia aliwahi kuvuma katika mziki wa Bongo fleva na vibao vikali amejifungua.Msanii huyo ambaye katika siku za hivi majuzi aliingia chimbo na kumpotea katika vyombo vya habari amejifungua mapacha wa kiume.K lyn ashawahi fanya collabo na wasanii kama vile Noorah,jay mo,squeeezer,bushoke na mr blue..

HII HAPA TRACK MPYA KUTOKA KWA MKALI C -SIR MADINI INAITWA PAIN KILLER

C-SIR MADINI - PAIN KILLER (TAMTAM)_Tete... in Hulkshare:

Tuesday 9 October 2012

VIDEO KALI KUUTOKA KWA BUGZ

HII HAPA TENA VIDEO WAZIMU KUTOKA KWA BOBBY MAPESA AKIWA NA MP VBO...NI KITU CHA KISHUA KUTOKA KWA WASHUA WA KWELI SI UNAJUA....HAWA JAMAAA WANAJIITA BUGZ ILA KUNA KIPINDI FLANI HIVI WALIKUJA WAKATENGANA NA KILA MMOJA WAO AKAAMUA KUFANYA SOLO PROJECT...KWA SASA WASHARUDI PAMOJA TENA NA TAYARI WASHAFANYA TRACK KALI KADHAA IKIWEMO HII HAPA INAYOKWENDA KWA JINA LA FANYA NA PIA KUNA NYINGINE INAJULIKANA KAMA MEZO....ENJOY HII VIDEO MARIDHAAAAAAAAAAAAAADI KABISA

Saturday 6 October 2012

OCPD WA GARISSA NA MAAFISA KUMI WA POLISI WAFUTWA KAZI

OCPD wa Garissa Felix munyambu na maafisa wengine wa usalama kumi wamefutwa kazi kwa tuhuma za kuruhusu washukiwa wawili wa kigaidi kuingia humu inchini na silaha hatari mnamo may tarehe nne mwaka huu.Mbali na munyambu,kuna maafisa wengine kumi waliofutwa kazi,sita wakitoka katika kitengo cha regular police huku wanne wakitoka katika kitengo cha AP waliokua wakishika doria katika kivukio cha Tana(tana bridge).Baadhi ya washukiwa wa ugaidi waliopita katika kivukio hicho cha tana walinaswa matuu wakiwa na kilo nane za vilipuzi,
waziri wa usalama Ole metito amewasihi maafisa wa polisi wawe wazalendo katika kazi yao ili waweze kuimarisha usalama wa wakenya.Metito pia alimuamuru kamishna wa polisi awapandishe ngazi maafisa walionasa vilipuzi huko matuu.

Friday 5 October 2012

Queen Darleen - Kokoro.mp3 in Hulkshare:

 Queen Darleen - Kokoro.mp3 in Hulkshare:

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA AMANI MJINI GARISSA




                                                  DUALE
                                       ERNEST MUNYI
Kutokana na kudorora kwa usalama katika mji wa Garissa,mkuu wa mkoa wa kaskazini 
mashariki bwana ERNEST MUNYI aliitisha mkutano wa dharura jana ili kuzungumzia 
uimarishaji wa usalama katika mji wa Garissa, Wakaazi wa mji wa garissa walialikwa
katika mkutano huo uliofanyika government guest house ili kutoa maoni yao.
Kilichojitokeza wazi katika mkutano huo ni kwamba chanzo cha uhalifu ambao umeshuhudiwa 
katika siku za hivi majuzi ni kutoaminiana baina ya serekali na wanainchi  mjini Garissa.
Wanainchi wanahoji kuwa wanaogopa kuwasillisha ujumbe wowote kwa polisi kisa eti wanaogopa 
kuwa huenda polisi wakayaweka wazi majina yao hadharani hivo basi kuyahatarisha maisha yao,
maafisa wa usalama kwa upande wao wamedaiwa kutoamini habari zinazotoka kwa wanainchi.
Mkutano huu umefanyika baada ya kushuhudiwa kwa visa kadhaa vya utovu wa usalama,
ikiwemo kuuwawa kwa maafisa wawili wa AP jumapili iliyopita.Pia bwana munyi aliamuru ukaguzi 
uimarishwe zaidi hasa katika kivukio cha mto tana na kuwaomba maafisa wa polisi kutozembea kazini.Kwa upande wake mbunge wa dujis alisema kuwa atatoa takriban shillingi millioni moja ili 
kufadhili ununuzi wa viti vya maafisa wa polisi vilivyo chomeka fedha hizo zikitoka katika hazina
 ya CDF emergency fund.

WITO UMETOLEWA KWA WANAINCHI KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA 
USALAMA ILI KUIMARISHA USALAMA MJINI GARISSA

By Jacob Musya Sifa f.m Reporter

Thursday 4 October 2012

JAMAA MMOJA HUKO CARLIFORNIA ACHEMSHA MAITI YA MKEWE KWA SIKU NNE

Koti moja huko california imempata na hatia  jamaa mmoja kwa jina la David Viens kwa kosa la kuichemsha maiti ya mkewe kwa siku nne na kuitupa ili kuficha ushahidi wa mauaji.Inasemekana viens alishtakiwa na kosa hilo ambalo alikiri wazi kotini kuhusika .Kulingana viens ni kuwa siku ya tukio alikuja nyumbani akakuta kuna fedha zake zimepotea hivyo basi akaanza kumkaripia mkewe huku akidai kuwa amregeshee fedha hizo akidai kuwa yeye ndio kaziiba.ni katika ugomvi huo ndio mkewe alikumbana na kifo chake.Ili kuharibu ushahidi,viens aliona cha kufanya ni kuuchemsha mwili wa mkewe alafu baadaye akaujumuisha na takataka zingine na kuutupa kama takataka

Wednesday 3 October 2012