Sunday, 19 July 2015
SARATANI INAYOUA MZIKI WA PWANI
Ni kwa siku nyingi saana mziki wa pwani umekua kaburini na unazidi kutapatapa kujitoa uonekane katika hatua za juu.Wengi wamejiuliza ni kipi kinachosababisha hali hii huku kukiwa na hali ya kurushiana lawama ila kulingana na upeo wangu mdogo wa mziki nilionao nahisi kwamba kila mshikadau kuanzia producer,watangazaji na ma DJ,wasanii wenyewe hadi mashabiki wote wamechangia katika hali hii.
MASHABIKI.
Labda nianze na shabiki,Ni kwa mda mrefu saana sasa msanii wa nyumbani amelalamika saana kwamba wewe shabiki unamnyima nafasi kwenye skio lako na kwamba nafasi hiyo umewapa wasanii wa magharibi mwa africa pamoja na marekani.Hii ni hali ambayo msanii wa pwani imezidi kumkatisha tama sana.Kufikia kiwango cha msanii Kaa La Moto kutunga wimbo uliokemea hali hii na kumhimiza kila mkenya kiujumla kuukumbatia na kuukubali mziki wa nyumbani kwanza kabla kuupa nafasi mziki wa mataifa mengine.Kwanza pongezi kwa msanii KAA LA MOTO kwa wimbo KLM IS DEAD,pili kwa tatizo hili lawama itaanguka popote pale iwe kwashabiki,presenters,DJS,Maproducer miongoni mwa washikadau wote katika sanaa. Anayebisha kuwa pwani hakuna vipaji ni muongo au kiufupi tuseme tu ana laana maana kwa upeo wangu mdogo wa muziki nilionao naweza kusimama mbele ya watu na kujivunia vipaji vya wasanii kama Ally B, Johnny Skani,Dazlah Kiduche,Majid,Susumila,Amoury beyby,Dogo Richie,Kaa la Moto,Nyota Ndogo,Lovemums, Jovial,Kigoto Mmbonde,Alkenia Love,Shaah Biggy,Chikuzee,Shembwana Masauti,Fisherman,Canibal,Sharama,Mchafuzy, Sudi Boy, Lai miongoni mwa wasanii kibao tu ambao kila siku wanakesha wakijaribu kila wanaloliweza kutupatia kazi nzuri na kuuweka mziki wa pwani katika ramani ya kitaifa na kimataifa kiujumla.

Ninachoamini ni kuwa wasanii wetu japo sio wote bali wengi
wao wana nia hivyo basi sisi kama mashabiki.Tukiwapa sapoti ni dhahiri kuwa
itawapa moyo wa kufanya bidii kuimarisha sanaa hii na kufikia viwango vya
kupendeza kila skio.Sijasema kuwa ususie kazi nzuri za wanamziki wa inje ya
pwani, hapana....ninachomaanisha ni kuwa tusiwe watumwa wa kiakili kupenda
zaidi vya wenzetu kufikia kiwango cha kudharau kazi nzuri za wasanii wa hapa
kwetu.
Nafasi iko kubwa ya kuimarisha uchumi wa sanaa yetu ya nyumbani na kabla nizungumzie fursa hizo kwanza kila shabiki anafaa kutambua kuwa sanaa ya kila msanii iko kwa mikono ya yeye shabiki,hivyo ina maana kubwa kuwa msanii hata awe na bidii kiasi gani bila shabiki ni dhahiri atafeli tu,maana katika kila kazi anayotoa msanii,ni lazima shabiki apate kuiskia,aipende na aipitishe moyoni mwake.Pia tunafaa kuelewa kuwa kumkubali na kumsifia msanii pekee hakutamuekea chakula mezani wala kumuimarisha kisanaa,shabiki anachofaa kutambua ni kwamba sanaa ni kazi wala sio ngazi ya kutengeneza maskini wenye umaarufu.Hivyo basi ni utovu mkubwa wa shukrani,unafik na kukosa uzalendo kama shabiki hatampa sapoti msanii wa nyumbani na kuhamisha sapoti hiyo kwa wasanii wa kigeni.Hapo ndio tunarudi tena katika zile fursa za kuukuza uchumi wa soko letu la mziki ambazo nimekudokezea hapo awali.
Naam,shabiki unafaa kutambua kuwa kwa kununua kazi za msanii,iwe ni kwa mfumo wa ulbum au mifumo ya kidijitali kama vilemkito,mdundo, miito ya simu pamoja na mifumo yote ya mitandao kunampa mapato makubwa saana msanii.Pia wewe kama shabiki ukijitahidi kuhudhuria matamasha ya wasanii wa nyumbani ni kitu kinachompa nguvu sana msanii na kumtengenezea maslahi yanayomuongezea mbolea katika safari yake ya mziki maana ni kupitia mapato haya ndio watajibidisha hata kujitangaza nnje ya pwani kupitia bidii ya kutoa mziki mzuri na video zilizo na ubora wa kimataifa.

MAPRESENTER NA MA DJ
Hawa ni washikadau wawili ambao ni nguzo kubwa saana katika mziki maana ndio wanaotegemewa na msanii kufikisha kazi kwa mashabiki na pia vilevile shabiki amewekeza uaminifu wake kwa wawili hawa kujua kwamba akihitaji mziki mzuri atakua anaupata kila siku kupitia kwao.Sanaa ikidondondokea pua lawama kubwa itawaendea wawili hawa,endapo sanaa itaimarika basi ni wazi kuwa asilimia kubwa ya sifa itawarudia wawili hawa.Naheshimu saana juhudi za DJs na PRESENTERS ila ujumbe unaofaa kuwaendea ni kwamba mziki m'bovu ni m'bovu tu hata uchezwe mara milioni kwa siku.Hakuna kitu kibaya kama kuona mziki unadidimia kila siku wakati mziki mzuri unanyimwa nafasi hewani huku mziki m'bovu ukipewa nafasi kisa upendeleo au mtu hongo.Ni picha ya kusikitisha kuona chat za top ten zikitawaliwa na nyimbo mbovu ambazo hata mtoto mdogo zitampatia uvivu wa kuzisikiliza kwa ubovu wake kisa mtu kahonga au pengine anapewa teke la "ushkaji".Hii ni hali inayouregesha mziki nyuma kwani ni utahira wa hali ya juu kuleta mazao yaliyooza sokoni tukiacha bidhaa nzuri zikiozea shambani.Ile siku DJ na PRESENTERwataweka tamaa kando na kuanzisha harakati za kuupa nafasi mziki mzuri na vipaji halisi hewani,hapo tutakua tumepiga hatua kubwa saana katika safari ya kuufikisha mziki wetu mbali.Kwa mtazamo wangu,upendeleo,ushabiki na "ushkaji" ni saratani kali saana inayoua mziki kwa kasi kubwa na wanaofaa kutibu saratani hii ni ma DJ pamoja na ma PRESENTER.Kivipi? kwanza kabisa kazi mbovu ni mbovu tu iwe imetoka kwa msanii mkubwa au mdogo,kama mtu amechemsha,amechemsha tu na anafaa kurekebishwa tuweke ushabiki kando,pili kuna watu wanaimba tu kisa mjombake au ndugu yake ni DJ au Presenter wa radio flani akijua wazi kwamba atapata shavu la kutoka kimabavu hata kama kipaji sufuri.

Upendeleo kama huu ukiuweka pembeni itakua tumepiga hatua nyingine kubwa katika
safari yetu ya mafanikio.Kwa mara nyingine nasisitiza kuwa pwani hakuna uhaba
wa mziki mzuri, hivyo basi hakuna sababu inayopelekea mziki m'bovu
kulazimishiwa maskio ya shabiki wakati kuna kazi nyingi nzuri zinazohitaji
nafasi katika soko letu la burudani. Tatu,Sioni sababu presenter
kuupa asilimia kubwa mziki wa mataifa ya magharibi katika kipindi chake na
kuitupa jalalani CD ya msanii wa nyumbani mwenye kipaji ambacho hakitaburudisha
tu mashabiki wa nyumbani bali pia kitapandisha uchumi wa sanaa yetu kwa kiwango
kikubwa.Ni kwa mara nyingi saana ma presenter mbalimbali wamejitokeza na kukiri
kuwa wanalazimika kuucheza mziki wa mataifa ya nnje kwa kisingizio kuwa
mashabiki huupendelea saana mziki huo zaidi ya ule wa nyumbani.Huu naweza
kusema kuwa ni uongo wa hali ya juu kwani shabiki kwa mara nyingi huzibwa macho
na hao ma presenter na kuaminishwa kwa nguvu kuwa wasanii wa nyumbani ni "kanjanja".
Hali hii hupelekea mashabiki kulazimishwa kuamini kuwa
kizuri pekee ni kile kigeni.Tunafaa kuelewa kwamba hao wasanii wageni ambao
tumewahusudu saana walipewa sapoti na kukubalika kwao kwanza kabla waote mbawa
za kuja kuusambaza mziki wao huku kwetu. Hivyo basi tunafaa pia sisi tuondoe
nidhamu ya uoga,tujiamini na kile tufanyacho,tujitahidi
kwa pamoja ili wasanii hao wageni wakija kwetu kujinadi pia sisi tuwe na vigezo
vya kwenda kujinadi huko kwao kwa kuuza kile kizuri tulichonacho.Hii yote
italetwa na juhudi za DJ na PRESENTER kuwapa sapoti wasanii bora na sio
bora wasanii.Mwiba wa mwisho ni huu hapa.Mtangazaji hafai
kujivika maringo mbele ya msanii,anachofaa kutambua ni kuwa sanaa imemsaidia
saana katika kazi yake.Utagundua kwamba mziki ni muhimu kwako wewe mtangazaji
endapo utavuta taswira ya kipindi cha top ten bila
muziki.hivyo basi mtangazaji elewa kuwa asilimia flani ya pato lako liko
mikononi mwa msanii.
MSANII
MSANII
Sasa hapa ndio shina kuu la sababu ya makala haya
lilipo.Kabla tuendelee namnukuu prof jay kwenye wimbo wa mtazamo akisema"sioni
sababu za msingi kuomba kwenye mitaa,kama una kipaji iweje ufe na njaa?" ila
katika wimbo huo huo pia namnukuu afande selle akisema "hivi ni
lazima sote tuwe wasanii,mimi nadhani imetosha wengine tuwe mashabiki".Hii
inaonesha wazi kwamba kila mmoja ana haki ya kuwa msanii kwani mziki
hauna mwenyewe,ila wasanii ni wengi ila wachache saana ndio wenye
vipaji.Talanta ni kitu cha msingi saana ambacho mtu anafaa kukitambua mapema
saana katika safari ya maisha yake.Inasikitisha kuona wasanii wengi wenye tungo
dhaifu wanalazimisha kitu ambacho ni dhahiri kuwa hawajahesabiwa na mungu kisa
ubishoo.Msanii yoyote ambaye yuko kwenye mziki kutafta umaaarufu anafaa kujua
kuwa anaishi katika upande usiofaa wa historia.Tunafaa kuelewa kuwa hata uwe na
nia kiasi gani kama talanta huna ya kuimba rudi nyumbani ukajifikirie tena ni
talanta gani ambayo mwenyezi mungu alikupa,kwani umaarufu ambao unautafuta
kwenye mziki unapatikana katika talanta zingine kwani kuna watu dunia hii
wamejenga jina na kuishi maisha mazuri kupitia uchoraji na hata kupiga marimba.
mwaka juzi kuna msanii kutoka kundi la MAKEKE FAMILY kwa jina RUDIWUU alitoa
dis track ambayo ilielekezwa kwa ma presenter inayoitwa HAKI NA USAWA na
kuiweka you tube.Kwenye ngoma ile RUDIWUU aliwatusi ma
presenter wengi mashuhuri matusi ya nguoni kwa kuwataja majina mmoja baada ya
mwingine akidai kuwa wanawanyanyasa wasanii wa nyumbani kwa kutowapa
airplay.Kwa mtazamo wangu wimbo ule kama ulikua unawakilisha kilio cha wasanii
wa pwani basi ni aibu kubwa saana kwa sanaa ya pwani kuwa na mabalozi kama
wale.Kwanza kabisa wimbo ulikua unaitwa "HAKI NA USAWA".
Ni haki gani hiyo anayoizungumzia?
Tunafaa kujua kuwa sio haki ya msanii kuchezwa kwa radio station,ingekua ni haki basi kesi zingekua zimejaa kortini au barabara zingekua haziishi maandamano.Sote tunafaa kuelewa kuwa katika hii safari Producer,msanii,presenter,DJ na shabikitunategemeana.Tunafaa kuelewa kuwa stesheni za runinga na redio vipo kibiashara,kujuza na kuelimisha huku fungu la msanii la kuburudisha likija mwisho kabisa.Mziki na burudani vinatumika tu kama kivutio kwa wasikilizaji.Hii inaonyesha wazi kuwa mmiliki atachagua kinachovutia kwa wasikilizaji wake ili kukidhi mahitaji ya ushindani mkubwa uliopo sasa katika sekta ya burudani na uanahabari.Jukumu lote hili la kuchagua kilicho bora kwa skio la msikilizaji linaanguka kwa mikono ya presenter.
Hivyo basi wewe kama msanii unafaa kuwajibika pia katika
harakati zako za kutoa mziki mzuri ambao utakua unamsaidia yule mtangazaji
pamoja na DJ kujenga jina kwa yule shabiki wanayemlenga.Kuna msemo unao sema
asiyefanya kazi naasile,vilevile msanii ambaye hatajitahidi katika ubunifu
hafai kuwa na nafasi katika skio la shabiki.
MSIKILIZE DAZLAH AKIZUNGUMZIA MZIKI WAKE PAMOJA NA COLLABO YAKE NA MSANII MKUBWA WA NAIROBI
Msanii kutoka studio ya TEE HITS kwa jina
la DAZLAH KIDUCHE huenda ikawa sio kichwa kigeni katika skio
lako kama wewe ni mfuatiliaji makini wa mziki wa pwani.Msanii huyu mwenye umri
mdogo saana amechipuka na kukua kwa kasi ya juu saana katika tasnia ya mziki wa
pwani na kufikia sasa, licha ya kuwa ni msanii aliyeanza mziki miaka ya
juzijuzi,kwa wakati huu amewapiku baadhi ya magwiji na kuandikisha jina lake
katika orodha ya wasanii wachache wanaowakilisha mziki wa pwani kitaifa na
kufikia sasa tunaweza kusema kimataifa
Katika siku za hivi majuzi msanii Dazlah ameonekana
kuwa mmoja ya wale wasanii wanaojituma saana na kuwekeza kwenye mziki kuanzia
upande wa studio,mauzo pamoja na kazi zenye akili ili kukidhi
mahitaji ya soko gumu la muziki.
Huyu apa dazlah msikilize akizungumzia mengi kuhusu mziki
wake, siri ya mafanikio yake pamoja na collabo yake na msanii mmoja maarufu wa Nairobi.
bonyeza hapa kumskiliza LISTEN
bonyeza hapa kumskiliza LISTEN
SABABU ZA ELIANO MTALIANO KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA
Ukiwa ni mwaka wa uchaguzi Tanzania,kumetokea wasanii
wengi wa mziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji kujitokeza na kutumia
umaarufu walionao kugombea nyadhifa mbali mbali za kisiasa inchini
Tanzania.Wasanii hawa ni kama vile a Prof Jay,Keisha pamoja na waigizaji steve
nyerere na wema sepetu.
Inaonekana hali kama hii huenda ikadhihirika wazi hapa
pwani kwani ikiwa ni mapema saana msanii wa injili kutoka hapa pwani
anayekwenda kwa jina mtaliano eliano amejitokeza na kuweka wazi azma yake ya
kuingia kwenye siasa mwaka wa 2017....huyu hapa msikilize akizungumzia ngazi ya
kiti atakachogombea,eneo analopania kusimamia pamoja na sababu zake za kujitosa
kwenye siasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)