Msanii kutoka studio ya TEE HITS kwa jina
la DAZLAH KIDUCHE huenda ikawa sio kichwa kigeni katika skio
lako kama wewe ni mfuatiliaji makini wa mziki wa pwani.Msanii huyu mwenye umri
mdogo saana amechipuka na kukua kwa kasi ya juu saana katika tasnia ya mziki wa
pwani na kufikia sasa, licha ya kuwa ni msanii aliyeanza mziki miaka ya
juzijuzi,kwa wakati huu amewapiku baadhi ya magwiji na kuandikisha jina lake
katika orodha ya wasanii wachache wanaowakilisha mziki wa pwani kitaifa na
kufikia sasa tunaweza kusema kimataifa
Katika siku za hivi majuzi msanii Dazlah ameonekana
kuwa mmoja ya wale wasanii wanaojituma saana na kuwekeza kwenye mziki kuanzia
upande wa studio,mauzo pamoja na kazi zenye akili ili kukidhi
mahitaji ya soko gumu la muziki.
Huyu apa dazlah msikilize akizungumzia mengi kuhusu mziki
wake, siri ya mafanikio yake pamoja na collabo yake na msanii mmoja maarufu wa Nairobi.
bonyeza hapa kumskiliza LISTEN
bonyeza hapa kumskiliza LISTEN
No comments:
Post a Comment