Sunday, 28 July 2013

DATA ZA MTUBEI NDANI YA SIFA PARADISE 29TH JULY 2013







































































































































TUSKER PREMIER LEAGUE RESULTS














Sun 28-07-13 AFC Leopards 1 0 Sofapaka Kasarani
Sun 28-07-13 Chemelil Sugar 2 0 Bandari Chemelil
Sun 28-07-13 KCB 2 2 Mathare United Kasarani
Sun 28-07-13 Western Stima 4 0 Thika United Bukhungu
Sat 27-07-13 Gor Mahia 2 1 Karuturi Sports City
Sat 27-07-13 City Stars 0 1 Ulinzi Stars Hope Centre
Sat 27-07-13 Sony Sugar 0 1 Muhoroni Youth Awendo
Sat 27-07-13 Tusker 1 0 Homeboyz








GARISSA




  • ujenzi wa mitaro kando ya barabara za mjini garissa unaondelezwa na wizara ya barabara mjini garissa itakayoelekeza maji ya mvua ndani ya mto tana..hii itakua afueni kwa maeneo yanayoathirika pakubwa na mafuriko haswa maeneo ya windsor.
  • je?..kwa upande wa kaunti ya tana river kuna njia gani ya kukabiliana na mafuriko yanayohangaisha wakazi wa kaunti hiyo?


  • baadhi ya taasisi zilizoihama garissa kwa sababu za usama kurudi tena baada ya utulivu kushuhudiwa
  • shughuli zaendelea kurudi katika hali ya kawaida katika mji wa garissa na huku biashara zikiendelea kunoga
  BURUDANI
  • HIP HOP DARASA NDANI YA SIFA PARADISE
  • TRACK MPYA KUTOKA KWA YOUNG D
  • MKALI WA RHYMES KATI YA DARASA NA STAMINA
  • LISHA NENO(KUJIFUNZA KUPITIA MZIKI WA HIP HOP)
HAMASA
  • JIFUNZE KUPITIA HUSTLER WA MTAA
  • RUDI SKONGA
  • NA MENGI KUTOKA KWA MP






NGOMA MPYA KALI KUTOKA KWA DOGO JANJA...BERRY BLACK FT ALIKIBA...YOUNG DEE

 DOGO JANJA-SEREBUKA

BERRYBLACK FT ALIKIBA-ISHARA



YOUNG DEE-KIJUKUU

KWA UBISHI NA HSIRA NARUDI TENA NDANI YA GAME "RAY C"

RAY C ATANGAZA KURUDI TENA NDANI YA MZIKI WA KIZAZI KIPYA MWEZI WA NANE ILI KUPAMBANA KUIMILIKI NAFASI ALIYOKUA NAYO KABLA HAJAATHIRIKA NA MADHARA YA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA...
                                      
CHINI NI MOJA YA VIDEOS ALIZOSHIRIKI KABLA HAJAKUBWA NA MADHARA YA MADAWA ALIPOSHIRIKISHWA NA MSANII LADY B KWENYE VIDEO YA MREMBO REMIX

WELCOME BACK MREMBO GAME BADO YAKUHITAJI...

BOB JUNIOUR-KIMBIJI


Wednesday, 19 June 2013

MGOMO WA WALIMU…

 
Masomo katika shule zote za upili za  uma katika kaunti ya Tana River na Garissa  yanaendelea hata baada ya mgomo kuitishwa  na chama cha walimu wa shule za upili cha KUPPET.
Hii imebainika baada ya uchunguzi Tuliofanya hapo jana. Katika baadhi ya shule tulizo tembelea  tulikuta masoma yakiendelea  kama  kawaida.Katika shule ya upili ya Garissa High naibu mwalimu mkuu  Bw. Abdikarim Mohamed alitueleza kuwa wana subiri usemi  na ufafanuzi  zaidi kutoka kwa chama chao cha KUPPET.Ingawaje shule tulizotembelea katika kaunti ya Garissa na Tana River zilikuwa zikiendelea na masomo kama kawaida,  muungano  wa KUPPET unasisitiza kuwa mgomo uko na utaendelea.Haya yakijiri viongozi wa muungano wa walimu: KNUT, walisema hawatafanya mazungumzo na serikali kuhusu pesa za marupurupu wanazo idai serikali.



CHANZO CHA MOTO ULIOTEKETEZA SOKO LA GARISSA

Moto uliyo teketeza sehemu ya soko Mugdi mjini Garissa huenda ukawa ulisababishwa na makaa ya moto ambayo hayakuwa yamezimwa.
Hii ni kwa mujibu wa wafanyi biashara wa soko hilo tulio zungumza nao. Mkasa huo wa moto uliotokea siku ya jumatatu usiku, uliteketeza mali ya thamani kubwa. …
Hata ingawa haijabainika haswa chanzo cha moto huo,  baadhi ya wafanyi biashara walioadhirika na moto huo, walisema kuwa mfanyi biashara mmoja ambaye  hupika na kuuza chakula cha Githeri  hakuzima gunia la makaa aliyoyanunua, kwani hakufahamu kuwa makaa hayo, yalikuwa bado yanawaka moto.
Hii ni mara ya pili sehemu ya  soko mugdi kuchomeka  kwani  mwaka uliopita soko hilo lilichomwa katika rabsha na mshike-mshike ya ukosefu wa usalama. Hii ilikuwa baada ya wanajeshi wawili kuwawa karibu na maeneo ya hospitali kuu ya Garissa.                 

GAWASCO YATAFUTA SULUHISHO LA SHIDA YA MAJI MADOGO


Kampuni ya kusambaza maji mjini Garissa, GAWASCO, iliandaa mkutano na wakazi wa Madogo hapo jana. Ni Mkutano  ulio-andaliwa katika hoteli moja eneo la Madogo, uliokuwa wa kutafuta suluhisho mwafaka kwa tatizo la maji, ambalo limekuwa likisumbua wakazi wa Madogo kwa mda mrefu.
Kati ya maswala yalioibuka ni swala tata la kulipa maji, yaani, BILLING, huku wakazi wakiomba mbinu mpya ibuniwe ya kulipisha maji. Kuhusu malipo ya maji ya jumla, yaani FLAT RATE, meneja wa biashara wa GAWASCO, bwana Abdirahim Sheikh Hassan alisema kwamba wateja ambao hawajapata maji, elhali malipo yao ni FLAT RATE, hawatalipia billi ya maji kwa wakati ambao hawajapata maji.

BUDGET YA TANARIVER KAUNTI…18 June 2013



Kaunti ya Tana River imetenga shilling million ishirini (20,000,000) kwa sekta ya elimu, shilling million saba (7,000,000) kwa sekta ya mifugo na shilling million mia mbili (200,000,000) kwa sekta ya usafi na maji. Haya yamejiri katika kikao cha kukadiria bajeti ya County ya Tana River kilicho andaliwa hapo jana katika ukumbi wa Madogo Social Hall.
Akiongea  wakati  wa kikao hicho naibu wa mwenyekiti wa kamati ya budget bwana HUSSEIN GOBU GODHANA, alisema kuwa afisi ya Gavana wa Tana River ingependa kuhusisha wananchi wote wa Kaunti hii katika bajeti hiyo.Na kwa upande wake mwakilishi wa ward ya Madogo, ABDI ERIGAMSO alikosoa bajeti iliyopendekezwa kwa kusema haikumhusisha mwananchi wa kawaida. Aidha Abdi Ergamso amesema bajeti hiyo haijatenga kando fedha za mikasa, kama vile mafuriko na baa la njaa. Akiongezea, Abdi Ergamso aliomba fedha zitengwe kwa ajili ya elimu ya chekechea akisisitiza elimu ya chekechea ndio msingi wa elimu.

Tuesday, 4 June 2013

REST IN ETERNAL PEACE ALBERT MANGWAIR

Watu wengi wajitokeza kuupokea mwili wa msanii wa bongo flava marehemu albert mangwea katika uwanja wa ndege

WAREMBO WAMAREKANI WAUIMBA WIMBO WA CHAMILLIONE BADILISHA A-Z

Hali hii inadhihirisha wazi kuwa sio lazima uimbe kiingereza ndio kazi yako itambulike ughaibuni,hatalugha zetu za africa pia zina utam wake

Friday, 22 February 2013

VIDEO YA TRACK MPYA YA OFFSIDE TRICK NA BABY J-USINIPE


COUNTY COMMISSIONER GARISSA:SERIKALI IPO IMARA KATIKA SWALA LA USALAMA WA GARISSA

County commissioner wa Garissa Bw Mohamed maalim amesema kuwa serikali ipo imara katika maswala ya usalama katika kaunti ya Garissa.Maalim amesema kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa usalama wa wakaazi wa Garissa umeimarishwa vilivyo huku akiwaomba wakazi wa Garissa kutoa habari zozote kwa maafisa wa usalama, na pia wakome kuwaficha wahalifu.Aidha maalim alisema kuwa kulingana na upelelezi ni kwamba zipo hospitali za kibinafsi zinazotoa huduma kwa wahalifu kwa kuwapatia matibabu wanapopata majeraha katika shughuli zao za uhalifu.Maalim amesema hospitali zitakazopatikana na makosa ya kuwatibu wahalifu zitafungwa mara moja.Pia amewahimiza wanainchi wa Garissa kuhakikisha kuwa wanadumisha amani haswa wakati huu tunapoelekea kwa uchaguzi huku akionya kuwa watakaozua vurugu watakiona cha mtema kuni kwani mkono wa sheria utakabiliana nao vilivyo.

ONYO KWA WAKAAZI WA GARISSA KUTOKA KWA MZALENDO KIBUNJA

Mwenyekiti wa tume ya uwiano na maridhiano NCIC Bw. Mzalendo kibunjia amewaonya wakaazi wa Garissa dhidi ya Ubaguzi wa kikabila,akizungumza katika mkutano  na wakaazi wa kaunti ya Garissa hapo jana.Mzalendo kibunjia alisisitiza kwamba ubaguzi wa wakenya haswa wale ambao si wa asili ya kisomali ni jambo ambalo halifai na linafaa kukemewa kabisa.Katika hotuba yake kibunjia aliwaomba wanainchi wa Garissa kupuuza matamshi ya baadhi ya watu na viongozi yanayosambaratisha uhusiano mzuri uliopo kati ya wakenya walio na asili ya kisomali na wale wasiokuwa wasomali huku akisema kuwa wakenya wanafaa kuwa mstari wa mbele kuheshimu na haki na maslahi ya kila mtu.