Monday, 22 October 2012

HALI ILIVYO KATIKA MTAA WA WINDSOR MJINI GARISSA




                                                HII NI BARABARA YA WINDSOR
                                                    HII NI COMPOUND YA MTU

                               HAPO SASA IKIFIKA HAJA KITAMBO UFIKE MSALANI NI BAALAA
Ni kwa mda sasa wakaazi wa mtaa wa windsor mjini Garissa wamelalamikia kuvuja kwa kwa mabomba ya maji taka(sewerage)kufikia sasa hali imekua mbaya saana kama unavyoona kwenye picha hapo juu ambapo sewerage hiyo imefikia kiwango cha kufurika hadi kuingia majumbani mwa watu haswa baada ya mvua kubwa iliyonyesha juzi.Kulingana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao nilipata fursa ya kuongea nao ni kwamba sewerage hiyo imekuwa shida kubwa saana kwa eneo hilo kwa mda sasa na inatoka katika louge moja iliyoko katika eneo hilo.Wakaazi hao wamesema wamewasilisha malalamishi kwa wamiliki wa nyumba ili ujumbe ufike katika afisi za town council ya Garissa ili swala hilo lishughulikiwe ila juhudi zao hazijafua dafu,Baadhi ya wakaazi wanasema kuwa mwenye louge hiyo ni mtu ambaye anajulikana na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa saana mjini Garissa.

Kufikia weekend iliyopita sewerage hii ilikua imefunga kabisa barabara na imetapakaa katika ploti kadhaa za makaazi.Uvundo unaotoka katika eneo hilo umezidi huku wenyeji wakihofia kuchipuka kwa magonjwa mbali mbali yanayotokana na maji machafu.Kwa sasa wakaazi wa eneo hilo wanaomba msaada kwa washikadau wa idara husika haswa town council na Gawasco  kuingilia swala hilo ili hali ya usafi irejeshwe katika mtaa huu kwani hofu kubwa ni pale mvua kubwa itakaponyesha huenda sewerage ikaingia mpaka majikoni.

No comments:

Post a Comment