Friday, 5 October 2012

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA AMANI MJINI GARISSA




                                                  DUALE
                                       ERNEST MUNYI
Kutokana na kudorora kwa usalama katika mji wa Garissa,mkuu wa mkoa wa kaskazini 
mashariki bwana ERNEST MUNYI aliitisha mkutano wa dharura jana ili kuzungumzia 
uimarishaji wa usalama katika mji wa Garissa, Wakaazi wa mji wa garissa walialikwa
katika mkutano huo uliofanyika government guest house ili kutoa maoni yao.
Kilichojitokeza wazi katika mkutano huo ni kwamba chanzo cha uhalifu ambao umeshuhudiwa 
katika siku za hivi majuzi ni kutoaminiana baina ya serekali na wanainchi  mjini Garissa.
Wanainchi wanahoji kuwa wanaogopa kuwasillisha ujumbe wowote kwa polisi kisa eti wanaogopa 
kuwa huenda polisi wakayaweka wazi majina yao hadharani hivo basi kuyahatarisha maisha yao,
maafisa wa usalama kwa upande wao wamedaiwa kutoamini habari zinazotoka kwa wanainchi.
Mkutano huu umefanyika baada ya kushuhudiwa kwa visa kadhaa vya utovu wa usalama,
ikiwemo kuuwawa kwa maafisa wawili wa AP jumapili iliyopita.Pia bwana munyi aliamuru ukaguzi 
uimarishwe zaidi hasa katika kivukio cha mto tana na kuwaomba maafisa wa polisi kutozembea kazini.Kwa upande wake mbunge wa dujis alisema kuwa atatoa takriban shillingi millioni moja ili 
kufadhili ununuzi wa viti vya maafisa wa polisi vilivyo chomeka fedha hizo zikitoka katika hazina
 ya CDF emergency fund.

WITO UMETOLEWA KWA WANAINCHI KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA 
USALAMA ILI KUIMARISHA USALAMA MJINI GARISSA

By Jacob Musya Sifa f.m Reporter

No comments:

Post a Comment