Thursday, 18 October 2012

SWALA LA VITAMBULISHO GARISSA NA MADOGO LACHUKUA MKONDO MPYA

Hili swala la vitambulisho sasa naona limeanza kuchukua mwelekeo mpya.Katika maeneo mengi Garissa,Mororo,madogo,tana river county na Garissa county kiujumla,kumekua na lalama kila uchao kuwa kupata kitambulisho ni balaa.Swala hili limekua likisumbua watu wengi saana haswa wakati huu  usalama umezorota ambapo wewe kama mkenya maisha ya Garissa bila kitambulisho ni balaa.Tukiweka hayo ya usalama kapuni jambo lingine la msingi ni kuwa uchaguzi mkuu unakaribia na endapo mkenya huna kitambulisho basi inamaanisha wazi kuwa hutaweza kupiga kura.

Wiki hii kumekua na pilka nyingi saana haswa sehemu za madogo na mororo kuhusu swala hili la vitambulisho baada ya jamaa mmoja kupiga simu siku ya jumanne katika kipindi cha BURUDANI KIKWETU Katika stesheni ya SIFA F.M na kutaja majina ya watu kadhaa kwamba walimlazimisha kulipa shilingi mia mbili ndio apewe kitambulisho.Swala hili limezua mjadala mkali na ilibidi tuweze kupata kauli ya D.O kuhusu jambo hilo ambapo alitaja kuwa huduma za kupata kitambulisho ni bure na hana habari yoyote kuhusu ada ya mia mbili inayotajwa kutozwa kwa wanaotafuta kitambulisho.

Siku ya alhamisi wazee kadhaa wanaohusika na maswala ya vitambulisho walifika katika afisi za Sifa f.m ili kuweka mambo wazi kuhusu swala hili la vitambulisho ambapo walisema kuwa wanajua wazi kwamba kupewa kitambulisho ni bure ila hao kama wazee walikaa na wakaunda kamati itakayoshughulikia swala hilo la vitambulisho,hivyo basi mtu yoyote anayetaka kitambulisho itambidi alipe shilingi mia mbili kama malipo kwa ile kamati,nanukuu mmoja akisema"HIYO PESA NI KAMA MAKARIBISHO TU YA ILE KAMATI,YAAANI TUSEME NI KAMA CHAI TU AU LUNCH"mwisho wa nukuu.Walipoulizwa huwa wanamsaidia vipi mtu anayetaka kufanya vetting na hana pesa,wazee hao walisema kuwa mtu ambaye hana mia mbili na anataka kuingia vetting huwa wanamsaidia mwisho anapata kitambulisho kwani kutoa hizo mia mbili sio lazima ni hiari ya mtu.

Baada ya wazee hao kutoka,kama sadfa kukaja kijana  katika Afisi za sifa f.m aliyesema namnukuu akisema"PESA TULITOA KUANZIA MWANZO NI MIA TATU MWANZO TULITOA MIA MOJA TUKAPEWA FORM TENA KWA VETTING TUKATOA MIA MBILI KWA JUMLA HIYO NI MIA TATU,NA HIZO PESA TULILAZIMISHWA KUTOA KWA SABABU WENGINE ILIBIDI WAACHE KITU KAMA SIMU HIVI NDIO WAWEZE KUHUDUMIWA HAPO KWA VETTING WAKIMALIZA WALETE PESA NDIO WACHUKUE SIMU ZAO"mwisho wa nukuu......
 Je mkweli ni nani katika sakata hii?
 hivyo ndio hali ilivyo kuhusu maswala ya vitambulisho kwa mengi zaidi ungana na Enos Changulo ndani ya changamka Sifa f.m 101.1 upate mengi kuhusu swala hili

No comments:

Post a Comment