Ni wiki ambayo imekumbwa na visa kadhaa vilivyoyumbisha usalama wa mji wa Garissa kwani toka jumapili basi wanaichi wamelazimika kuzishikilia roho zao mikononi kwani kila tu kiza kinapoingia jipya lakutisha na kuogofya linajiri.Siku ya jumapili usiku wa takriban saa tatu askari wawili wakapoteza maisha yao huko barabara ya ngamia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana,siku ya jumatatu ikawa zamu ya kituo cha polisi huko bula iftin ambako kulivamiwa na watu wasiojulikana.Siku ya jumanne moto mkubwa ukaunguza kituo cha polisi cha Garissa huku chanzo cha moto huo hakijulikani.Hali hii imesababisha taharuki baina ya wenyeji huku baadhi wakiuliza"kama wanaotulinda sisi wanaichi ndio wanauawa,je usalama wa mwanaichi wa kawaida upo kweli?Ni kwa sababu ya visa hivi ndio mkuu wa mkoa wa kaskazini mashariki bwana Ernest munyi amewapa makataa ya wiki mbili wanainchi wote walio Garissa na hawana vitambulisho wafanye iwezekanavyo kupata vitambulisho ...kwani baada ya wiki mbili kutakua na msako mkali.Kama huna kitambulisho unahimizwa ufanye iwezekanavyo upate kitambulisho maana msako huu utakapoanza basi sheria itachukua mkondo wake.
POPOTE ULIPO MKAAZI WA GARISSA HAKIKISHA UNADUMISHA AMANI
No comments:
Post a Comment