Leo tukajipata MCHELELO FARM moja ya mashamba yaliyoko kando ya mto
tana.Tumetambua huko maskani maswala na ukulima yamepewa kipau mbele
saana.Washkaji kibao wanautumia vizuri mto tana ndio maana licha ya jua
kali linalowaka tana river na Garissa kiujumla bado kuna uwezekano wa
kupata mimea mingi saana ikifanya vizuri katika maeneo haya yaliyo kando
na mto na hata yale yaliyombali iwapo tutakumbatia ukulima wa
unyunyiziaji maji kutoka mto huo.Kulingana na hali ilivyo katika kingo
za mto tana ni kwamba vipo vipande vingi saana vya ardhi ambavyo endapo
vitatumiwa vizuri basi tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo ya Tana
river na Garissa litapungua kwa kiwango kikubwa saana.Ndani ya mchelelo
farm kuna mimea mingi saana kama vile
sukuma,mchicha,mabiringanya,mabamia/mabenda,Tomato,mahindi,ndizi,vitunguu,miwa
na mimea mingi saana ikiwa ni dhihirisho kubwa kuwa ardhi hii iko na
rutuba ya kutosha kuweza kuhimili ukuaji wa mimea mingi tofauti.Hata
hivyo kila kizuri huwa hakikosi changamoto kwani mbali na kuwepo kwa unawiri
mzuri wa mimea tatizo ni kwamba zao lao mara nyingi huharibika shambani
kwa sababu wa uosefu wa wanunuaji kwani eneo hilo ni mbali saana na
sokoni hivyo basi zao linapokua tayari mara nyingi huozea shambani kwani kulifikisha
sokoni huwa ni ngumu saana...HIZI HAPA BAADHI YA PICHA ZA ENEO HILO
TANA RIVER
NDIZIMIWA
PUMPKINS
VITUNGUU
MAHINDI
MABIRINGANYA
TOMATO
SUKUMA
NIKAAMUA PIA KUPOZ NA WAKULIMA WENYE
KUSABABISHA USTAWISHAJI HUU
No comments:
Post a Comment